Na Nasra Ismail, Geita
MBUNGE wa Jimbo la Busanda Tumaini Magesa ameahidi ndani ya mwezi mmoja na nusu anatarajia kukamilisha ujenzi wa bweni katika shule ya sekondari Lutozo iliyopo katika Mamlaka ya Mji mdogo wa Katoro mkoani Geita.
Ametoa ahadi hiyo leo aliposhiriki kuchimba msingi wa bweni hilo ambalo linatakiwa kutumika katika msimu mpya wa masoma ya kidato cha tano mwaka huu.
Shule ya Sekondari Lutozo imekuwa ikifanya vizuri katika matokeo ya kidato cha nne kwa takribani miaka 5, hivyo kufanya shule hiyo kupata hadhi ya kuwa na masomo ya kidato cha tano na cha sita.
Magesa pia alipata wasaa wa kusikiliza kero za wananchi ambapo kero kubwa ni utiririshwaji wa maji yenye kemikali kutoka kwenye maplanti kwenda kwenye mito ya maji ya matumizi ya binadamu.
Ambapo Mbunge Magesa ameahidi kuita wataalam kupata majibu kuhusu usalama wa maji na pia kuongea na wamiliki ili waweze kuzuia utiririshwaji huo.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Katoro Kigongo Benedict Sweya amemshukuru na kumpongeza mbunge huyo kwa kutoa Sh.5 kutoka kwenye mfuko wa jimbo kwa ajili ya kuanza ujenzi wa bweni hilo.
"Matarajio ni kwamba mwaka huu tunaenda kupokea watoto wa kidato cha tano nina imani umewapigia wadau na wamekubali kushiriki kwani wana imani kubwa na wewe Mbunge wetu na ndani ya mienzi hiyo ujenzi utakuwa umekamilika,"Kigongo.
Aidha amemuomba mbunge kuwasaidia kupata kisima cha maji katika shule hiyo kwani imekuwa changamoto kubwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...