MITAA iliitika mitaa ikaukubali mziki wa Magwiji wa Odds kubwa, Nyumba ya Mabingwa wa michezo ya ubashiri na kasino ya mtandaoni, ufalme wa washindi Meridianbet pale walipopita mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar Es Salaam na kuwashika mkono wapambanaji wote.

Watu wengi walijitokeza kuona ni nini Meridianbet wamewaletea na hapo ndipo tabasamu lilipofunguka mithili ya jua la asubuhi linavyochomoza, mitaa na chocho zote za Jiji la bata na salama, liliguswa kwa kupatiwa nguo za kujikinga na mvua kwa Bodaboda na abiria wote, wafanyabiashara mbalimbali nk 

Kwa niaba ya madereva bodaboda na bajaji muwakilishi wao aliyefahamika kwa jina moja la Athuman alisema “Meridianbet hakika ni mwanga wa kila mtu na leo kila mtu anafaidika na msaada huu”

Meridianbet imetoa msaada wa nguo za kujikinga na mvua kwa madereva Bodaboda na Bajaji, wafanyabiashara wa sokoni ikiwa ni sehemu ya kupambana na madhara yatokanayo na mvua zinazoendelea kunyesha katika Jiji hili la Dar Es Salaam. Kwa upande wa muwakilishi wa Meridianbet alisema kwamba;

“Kampuni inatambua mchango wa madereva hao, na hivyo wameamua kuunga juhudi zao kwa kutoa msaada wa nguo hizo ili kutoathiri kazi yao kipindi mvua inaponyesha, pamoja na madhara ya kiafya yatokanayo na kunyeshewa na mvua”

Meridianbet ni kampuni inayofanya shughuli za ubashiri mitandaoni, na michezo ya kasino ya mtandaoni, kila siku washindi wengi wanajizolea mamilioni na kutajirika, pamoja na yote hurudisha kwa jamii kile wanachokipata.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...