Na Muheza


Madereva wa bodaboda wilayani Muheza wamekiri kuwa kundi hilo limekuwa sehemu ya vyanzo vya ajali za barabara kutokana na ukosefu wa  elimu ya usalama barabara miongoni mwao.

Kauli hiyo wameitoa wakati wa kampeni ya kutoa elimu ya  ya usalama barabara katika eneo la Mkanyageni barabara kuu ya Tanga Segeta iliyoendeshwa na kikosi Cha usalama barabara wakishirikiana na shirika la Amend.

Walisema kuwa wengi wao wamejifunza uderava wa vyombo hivi mitaani bila ya kwenda darasani kwa ajili ya kupata elimu sahihi hatua ambayo imekuwa ikiwasababishia wao kuwa visababishi vya ajali za barabara 

"Licha ya kazi hii kuwasehemu ya vipato vyetu lakini changamoto iliyokuwepo hatuna elimu ya usalama barabara lakini tunashukuru kwa hii kampeni hii imeweza kutupatia mwangaza wa umuhimu wa kuwa na elimu ya usalama barabara hususani katika matumizi ya vyombo vya moto uwepo barabarani"alisema Meshark Mhando 

Nae Kaimu Mkuu wa usalama barabara wilaya ya Muheza DTO Herberth Kazonde  alisema kuwa Kwa ufadhili huo wa ubalozi wa Uswizi kupitia shirika la Amend elimu hiyo wanayoitoa itaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza ajali sambamba na makosa mbalimbali ya barabara ambayo yangeweza kuzuilika.

Hata hivyo alisema kuwa kupitia kampeni hiyo wanayoitoa ni Imani yao kama kikosi Cha usalama barabara kuhakikisha bodaboda wanakuwa kundi salama kwani Sasa litakuwa na watu ambao ni waelewa tofauti na hapo awali .

"Kampeni hii tayari imeanza kuleta matunda katika maeneo ambayo elimu imeshafika kwani makosa ya barabara yameweza kupungua kwa kiwango cha kuridhisha hivyo tunawashukuru ubalozi wa Uswizi kwa kuja na mradi huu wa Elimu ya usalama kwa kundi hili la bodaboda"alisema.

Nae Mratibu wa mradi huo kutoka shirika la Amend Ramadhani Nyaza alisema kuwa Kwa kushirikiana na Jeshi la polisi waliona wapeleke kampeni hiyo katika eneo la Mkanyageni kwani limeoneka ni hatarishi kwa ajali za barabara 

"Tumekuja kutoa elimu ya usalama barabara ambapo tumewafundisha umuhimu wa wao kuhakikisha wanakuwa salama muda wote wanapotumia vyombo vya moto lakini na kuzingatia usalama wa watu wengine wanaotumia barabara hiz"alisema Nyaza.





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...