Na Janeth Raphael -MichuziTv -Dodoma

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Raisi Mipango na Uwekezaji Mhe Prof. Kitila Mkumbo amesema kuwa hatua ya kwanza kujipima katika maendeleo ni kuwa na usalama wa chakula na wakati tumeungana na Zanzibar usalama wa chakula ulikuwa asilimia 60 huku lengo la nchi ni kujitosheleza kwa asilimia 100 na kuwa na akiba lakini kwasasa Nchi jna usalama wa chakula kwa asilimia 124.

Waziri Prof.Mkumbo ameyasema hayo Jijini Dodoma katika mkutano wake na Wanahabari wakati akielezea mafanikio ya Wizara hii kuelekea Maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanzania.

Na kuongeza kuwa hatua ya pili ni katika ustawi wa na Nchi kwa kuzungatia mambo ya msingi ya kibinadamu ikiwemo chakula,mavazi na malazi ambayo nayo tumepiga hatua.

"Hatua ya kwanza kujipima katika maendeleo ni kuwa na usalama wa chakula. Wakati ule tumeungana, usalama wa chakula ulikuwa asilimia 60 huku lengo la nchi ni kujitosheleza kwa chakula kwa asilimia 100 na kuwa na akiba. Kwa sasa nchi ina usalama wa chakula kwa asilimia 124".

"Hatua ya pili kujipima katika maendeleo ni ustawi wa watu na nchi kwa kuangalia mambo ya msingi ya kibinadamu ikiwemo chakula, mavazi na malazi ambayo nayo tumepiga hatua kubwa".

Sambamba na hayo Waziri amesema kuwa yaliyopo ni kuwa ifikapo 2025 wastani wa umri wa kuishi kwa Watanzania uwe ni 68 japo kwa Sensa ya watu na makazi mwaka 2022 wastani wa kuishi ni miaka 66. Tukilinganisha wakati tunapata Uhuru ilikuwa ni wastani wa miaka 32.

"Wakati tunapata Uhuru, umri wa kuishi kwa Mtanzania ilikuwa wastani wa miaka 32, mwaka 2000 umri wa kuishi ukasogea hadi wastani wa miaka 52. Tamaa yetu ifikapo mwaka kesho 2025 wastani wa kuishi uwe miaka 68. Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, wastani wa kuishi ni miaka 66".

Kwa upande wa Elimu amesema kwa mwaka 2000 nchini Tanzania kiwango cha kuandikisha wanafunzi kilikuwa asilimia 69 lakini ya maendeleo ya taifa ya kwama 2025 ni kufikia asilimia 100 ya uandikishaji.

"Mambo matatu ya kufanya kukuza ustawi wa binadamu ni kumpa binadamu elimu ili aweze kuishi vizuri ambapo mwaka 2000 nchini Tanzania, kiwango cha kuandikisha wanafunzi kilikuwa asilimia 69. Kwa malengo tuliyojiwekea kwenye Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025, ni kufikia asilimia 100 ya uandikishaji wa wanafunzi ambapo hadi sasa tumevuka malengo, tupo asilimia 108.5".

"Kuhusu suala la kwenda sekondari, mnamo mwaka 1964 ilikuwa asilimia 5, mnamo mwaka 2000, watoto waliofanikiwa kufika sekondari kutoka shule za msingi ilikuwa chini ya asilimia 20. Lengo letu ifikapo mwaka 2025, tuwe tumefika asilimia 48. Kwa takwimu za hivi sasa, tupo asilimia 70".

"Dira ya Maendeleo ya Taifa inayokuja, tutahitaji elimu ya msingi Tanzania iwe kwa Watanzania wote na wote lazima kufika sekondari kwa asilimia 100".

"Eneo la pili la kukuza ustawi wa binadamu ni afya hasa kwenye eneo la mama na mtoto, na la tatu ni maji ambapo wakati tunapata uhuru, uwepo wa maji vijijini ulikuwa chini ya asilimia 15 na mwaka 2000 ilikuwa asilimia 32. Kwa sasa ni asilimia 77".

Waziri amemaliza kwa kusema kuwa Tuna mengi ya kujivunia katika muungano, tumefanikiwa kuzikabili na kuzitatua changamoto zilizojitokeza. Serikali imejidhatiti kupambana na changamoto zitakazojitokeza ambazo zitatishia muungano wetu.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...