-Yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Na Mwandishi Wetu

BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limewaonya watu wanaojenga miradi bila kupata Cheti cha Tathmini ya Mazingira EIA kwenye baraza hilo kwamba wanakabiliwa na faini ya shilingi milioni kumi.

Hayo yamesemwa leo Aprili 19,1024 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam na msosholojia wa Baraza hilo Suzan Chawe alipokuwa akizungumza kwenye ufunguzi wa maonyesho ya kumbukumbu ya miaka 60 ya Muungano

Maonyesho hayo yamefunguliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Abdulla.

Suzan amesema NEMC imekuwa ikifanya kaguzi za mara kwa mara na wale wanaokutwa wamejenga miradi bila EIA wamekuwa wakitozwa faidi inayofikia hadi shilingi milioni kumi

Amesema NEMC imekuwa ikiendesha kampeni ya elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa EIA kwa wanaojenga miradi kabla ya kufanya kaguzi na kuwatoza faini.

"Mfano unaweza kukuta mtu anajenga kituo cha mafuta kwenye makazi ya watu jambo ambalo ni hatari kama ikitokea dharura tunaweza kupoteza maisha ya watu kwa hiyo tunasisitiza umuhimu wa EIA kabla ya kuanza shughuli za ujenzi," amesema Suzan

Amesema kwa miaka 60 ya Muungano NEMC inajivunia mambo mengi ikiwemo kupigania ustawi wa mazingira kwa kuhakikisha miti mingi inapandwa na kulindwa.

Suzan amesema Baraza limefanya maboresho ya mifumo yake ya mapito ya taarifa za tathmini na kaguzi za athari kwa mazingira kwa kuimarisha miundombinu ya TEHAMA kulingana na matakwa ya mfumo wa serikali mtandao.

Amesema NEMC inasimamia miradi inayofanya tathmini ya athari kwa mazingira kwa njia ya kielektroniki kupitia usajili wa mtandaoni njia ambayo inamuwezesha mwekezaji kuanzisha mchakato wa kupata cheti cha EIA kupitia mfumo wa usimamizi wa mradi ( Project Management System).

"Kabla ya kufanya usajili wa mradi mwekezaji anatakiwa kuhakikisha mawazo ya wadau yamepatikana kuhusu utekelezaji wa mradi kwenye eneo husika" amesema Suzan.

 

Maofisa wa BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), wakihudumia watu waliofika leo kwenye viwanja vya mnazi mmoja Dar es Salaam kwenye maonyesho ya miaka 60 ya ya Muungano. Maonyesho hayo yamefinguliwa leo Aprili 19,2024 na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Abdulla

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...