Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi amewashukuru Masheikh na Waalimu kwa kazi kubwa ya kuendesha madarasa ya mawaidha katika Misikiti mbalimbali na Mihadhara kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo katika Baraza la Eid ukumbi wa Ziwani Chuo cha Polisi, Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 10 Aprili 2024.
Aidha Rais Dk.Mwinyi amewahimiza waumini wa Dini ya Kiislamu kuyaendeleza mafunzo waliyopata kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kudumu kufanya mambo ya heri na kuacha kutenda maovu katika maisha ya kila siku.

Rais Dk.Mwinyi ameliagiza Jeshi la Polisi kuhakikisha wanasimamia hali ya ulinzi na usalama wa barabarani kipindi hiki cha Sikukuu .
Vilevile amewaomba viongozi wa Dini kuendelea kuiombea Dua nchi na viongozi wake pamoja na kuendelea kudumisha amani na utulivu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...