Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe January Makamba leo tarehe 17 Aprili 2024 akiwa jijini Ankara, Uturuki ametaangaza kuhusu uamuzi wa Baraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili kwa ukubwa nchini Uturuki wa kumtunuku Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Shahada ya Heshima ya Udaktari katika Uchumi.

Amesema kuwa, Baraza hilo limefikia uamuzi huo kwa kwa kauli moja kutokana na kutambua Uongozi wake wa kipekee ambao umeleta mageuzi makubwa ya kijamii, kisiasa, na kiuchumi nchini Tanzania. Mageuzi hayo yameboresha ustawi wa Watanzania; na kuimarisha sifa ya Tanzania ulimwenguni; na yamekuza mahusiano ya kibiashara, kiuchumi na kisiasa kati ya Tanzania na nchi nyingine, ikiwemo Uturuki.

Hafla ya kukabidhiwa tuzo hiyo itafanyika kesho, tarehe 18 Aprili 2024, saa sita mchana, katika Chuo Kikuu cha Ankara na itaongozwa na Prof. Necdet Ünüvar, Mkuu wa Chuo, na kushuhudiwa na Wahadhiri na wanafunzi wa Chuo hicho. Pia, hafla hilo litahudhuriwa na Mabalozi wa nchi za Afrika wanaowakilisha nchi zao Uturuki.

Baada ya tukio hilo, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ataelekea katika Ikulu ya Uturuki na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Uturuki Mhe. Recep Tayyip Erdoğan kwa mazungumzo rasmi na Dhifa ya Kitaifa. Kisha, Rais Samia Suluhu Hassan ataelekea jijini Istanbul, mji mkuu wa kibiashara wa nchi ya Uturuki, kwa ajili ya kushiriki kwenye Kongamano la kibiashara la Tanzania na Uturuki, ambalo pia litahudhuriwa na Makamu wa Rais wa Uturuki.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...