Na Mwamvua Mwinyi,RufijiApril 23

Patrick Golwike (Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Mahitaji Maalum [WMJJWM]) ameridhishwa na misaada inayoelekezwa na huduma zinazoelekezwa kwa akinamama waliojifungua na watoto waliokumbwa na maafa ya mafuriko Rufiji na Kibiti mkoani Pwani.

Aidha amepongeza mkoa,maofisa ustawi wa jamii kata,wilaya na mkoa kwa namna wanavyosimamia  makundi ya Wanawake waliojifungua, wenye watoto na vijana wa kike ambao wapo kwenye ukuaji.

"Nichukue fursa hii pia kuwapongeza watalaam wa Maendeleo ya Jamii wakiongozwa na Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Pwani ambae ni mratibu wa Maafa Mkoa wa Pwani Roseline Kimaro ,ambao wamekuwa wakitekeleza jukumu la uratibu  wa kuhakikisha waathirika wa mafuriko katika kambi Tano zilizopo kibiti na Ruiji wanapata huduma za msingi hasa wanawake ,watoto,wazee,na wenye  mahitaji maalumu."alifafanua.

Hata hivyo kuhakikisha huduma za msingi zinatolewa kwa makundi hayo, mabinti balee kujilinda ,ulinzi wa watoto na kutoa elimu ya lishe na saikolojia  .

Nae Mratibu wa maafa Roseline Kimaro alifarijika kuona wadau ambao wanapeleka misaada muhimu hasa kwa akinamama waliojifungua , watoto na mabinti balee.

"Ninawashukuru na umoja wa wanawake Tanzania, na mkoa kwa kujitoa kwao kupeleka mahitaji muhimu ya wanawake ikiwemo pedi,pempas,mabeseni,,nguo ,vyombo na vyakula kwani ni kama walijua kwamba ni moja ya changamoto ambazo ziliainishwa kuwakabili wanawake na watoto "alibainisha Roseline.

Roseline aliomba wadau wa jamii kuendelea kuwakimbilia kundi la wanawake, watoto,vijana na akinamama wajawazito na waliojifungua ili kuwapunguzia changamoto zinazowakabili.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...