Na Said Mwishehe Michuzi TV

KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Salum Hapi amemshukuru Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuchukua jina lake na kunteua katika nafasi hiyo huku akieleza uteuzi wao waliongozwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho dk.emmanuel Nchimbi na Katibu wa Itikadi na Uenezi Amoss Makala ni Supar Sub.

Hapi ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam ambako zimefanyika sherehe za mapokezi ya Katibu wa Itikadi na Uenezi Amoss Makala,Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara John Mongela,Katibu Mkuu Jumuiya ya Wazazi Salum Hapi pamoja na Katibu Mkuu Jumuiya ya Vijana Jokate Mwegelo.

Akizungumza mbele ya mamia ya Wana CCM waliongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Abass Mtemvu ,Hapi ameenza kwa kutoa shukrani kwa Mwenyekiti wa CCM na Rais Dk Samia kwa kuchukua jina lake na kulipitisha CCM ili aweze kumsaidia na kukikasaidia Chama.

"Wazazi ndio tunalea vijana,tunaelea wanawake,tunakazi ya kuandaa chipukizi,vijana na akina mama.Shukrani zangu za dhati naomba nipeleke kwa halmashauri Kuu kupitisha jina langu.Nilitoka katika Chama baadae nikaazimwa serikalini...

"Na sasa nimerudi katika Chama na kwa lugha rahisi vijana wa mjini wanasema kisu kimerudi kwenye yala yake.Nataka niwahakikishie jumuiya ya wazazi na wana CCM kwa ujumla kuwa niko tayari kufanya kazi wakati wote kwa maslahi ya Chama na wasiwe na mashaka.

"Niahidi umuiya ya wazazi tunakwenda kufanya kazi usiku na mchana, hivyo jumuiya nyingine ziamke kwani kama baba alilala sasa ameamka.Mwaka huu ni mwaka uchaguzi wa Serikali za Mitaa.Hivyo jukumu letu ni kuhakikisha tunakwenda kutengeneza mazingira yatakayowawezesha CCM kushinda kwa kishindo katika Uchaguzi wa Serikali za mitaa na mwakani katika Uchaguzi Mkuu."amesema Hapi.

Ameongeza kuwa alichokifanya Rais Samia ni kuongeza mashambulizi ya timu ,Rais ni kama kocha basi alichofanya ni Super Sub."Timu inapokuwa uwanjani kocha huwa anasoma michezo, hivyo aliingiza Super Sub ya kwanza Katibu Mkuu Dk.Emmanuel Nchimbi.

"Na sasa amefanya Super Sub nyingine ya Katibu wa Itikadi na Uenezi Amoss Makala, Naibu Katibu Mkuu Bara John Mongela,Katibu Mkuu Jumuiya ya Vijana Jokate Mwegelo na yeye.

Tunafahamu Super Sub ya dakika za nyongeza huwa hatari sana katika kufanya mashambulizi na kupata ushindi,"amesema Hapi.

Pamoja na hayo ametumia nafasi hiyo kupeleka salamu kwa vyama vya upinzani kutambua huu sio wakati wa huruma kwani Rais Samia ametoa uhuru kwa wanasiasa kufanya siasa zao kwa uhuru ikiwemo kufanya mikutano ya hadhara 

"Wapinzani wasitegemee huruma, uchaguzi ni kushika dola, mikutano wote tunafanya,wote tumejipanga.Huu si wakati wa huruma,wapinzani wakapambane."







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...