NA.MWANDISHI WETU

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama amesema uwepo wa Kongamano la kitaifa la Ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya Kimkakati na Uwekezaji ni maono na maelekezo ya Mheshimiwa Rais na nimipango inayoendana na Dira ya Taifa.

Waziri amesema hayo leo tarehe 28 Aprili, 2024 Jijini Dar es salaam wakati akimkaribisha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko Kufunga Kongamano hilo lililoandaliwa na Baraza la Uwekezaji wa Wananchi Kiuchumi (NEEC).

Waziri alieleza kuwa Serikali itaendelea kutengeneza mazingira wezeshi kwa Watanzania ili kupata fursa ya kushiriki katika shughuli za kiuchumi; kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja, na kutengeneza uchumi jumuishi utakao inua uchumi wa Taifa kwa ujumla.

“Mhe. Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan amekuwa mfano wa kuigwa kwa hekima na busara katika kufanya mamuzi ndani ya Serikali yanayojumuisha makundi yote, na jambo hili tunalolifanya linaakisi maono yake ya falsafa ya R4,” alieleza Waziri Mhagama.

Aidha akieleza kuhusu Mkutano huo alisema unatija kubwa kwa ustawi wa taifa na kusisitiza kuwa utaendelea kuitishwa ili kuhamasisha, kuhimiza na kujenga uelewa wa pamoja ili kuongeza nguvu katika suala zima la uwekezaji.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akitoa neno la kumkaribisha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko katika kongamano la kitaifa la ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya kimkakati na Uwekezaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...