Na Mwamvua Mwinyi, Rufiji



Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyama Pori Tanzania (TAWA) imetoa misaada mbalimbali ikiwemo unga tani 6.4, maharage kilo 666, magodoro 186 vyenye thamani ya 20mil kwa ajili ya waathirika wa mafuriko wilayani Rufiji.

Aidha imetoa imetoa boti moja kwa ajili ya kuongeza msaada kwa vyombo vya uokoaji.

Akimkabidhi msaada huo Mkuu wa Mkoa wa Pwani alhaj Abubakar Kunenge, kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi (TAWA), Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania (TAWA) Kanda ya Kusini Mashariki SACC ,Abraham Jullu, alitoa pole kwa wananchi wa Rufiji na Kibiti .

Alieleza, licha ya msaada wa chakula na magodoro mamlaka hiyo imetoa boti ili kuongeza msaada kwa vyombo vya uokoaji na kusema kwamba wameendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya tahadhari ya wanyama ( mamba na viboko).

Alifafanua ,hadi kufikia aprili 15,2024 wametoa elimu kwa wananchi 4,226 katika kata nne wilayani Rufiji.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Pwani Kunenge alitoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Mamlaka hiyo chini ya usimamizi wa Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi (TAWA) Mej. Gen. Hamisi Semfuko na Kamishna wa Uhifadhi (TAWA) Mabula Misungwi kwa namna ambavyo (TAWA) ilivyojitoa kushirikiana na wananchi wa Rufiji na Serikali katika athari za mafuriko.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Meja Edward Gowelle aliishukuru TAWA kwa kuwa karibu na wananchi wa Rufiji hata kabla ya athari za mafuriko huku akimtaja Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mohamed Mchengerwa kuwa ndiyo kinara wa ushirikiano huo kati ya Taasisi mbalimbali na wadau wa maendeleo.

Wakati huo huo, Mbunge
wa Jimbo la Kibiti, Twaha Mpembenwe, amewataka wananchi waliozingirwa na mafuriko kuhama na kuepuka maafa makubwa yanayoweza kutokea kutokana na mvua kubwa inayo endelea kunyesha.

Aliyasema hayo akiwa katika ziara ya kuwatembelea wananchi wa jimbo hilo waliokumbwa na mafuriko na nyumba, mazao na mali zao kuzama hivyo kukosa mahali pa kuishi na malazi.

Akiwa katika kata ya Mtunda, iliyozingirwa kabisa na maji Mpembenwe aliwahakikishia wananchi hao kuwa serikali chini ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan,itasambaza misaada muhimu kupitia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kibiti.

Mpembenwe amesema licha ya misaada hiyo pia usafiri upo kwa wananchi waliotayari kuhama kwenda katika Kambi maalumu Ikwiriri ama Kibiti.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...