Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Tanzania Breweries (TBL) ambayo ni Moja ya watengenezaji wa bia na waajiri wakubwa nchini Tanzania na mshirika muhimu katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya nchi, leo wamesaini makubaliano na CRDB Bank Foundation ya kutekeleza kwa pamoja mpango wa kufadhili mradi wa mbegu kwa wakulima wa shayiri.

Ushirikiano huo, unaotokana na mradi wa kilimo stahimilivu wa TBL, unawakilisha hatua muhimu katika juhudi za kampuni ya TBL za kukuza kilimo endelevu kitakacho wawezesha wakulima kote nchini.

Mpango huu wa Kilimo Bora(Smart Agriculture) wa TBL, una lengo la kuwawezesha wakulima wake moja kwa moja hadi asilimia 100 ifikapo mwaka 2025,Mkakati huu utahakikisha wakulima wanakuwa na ujuzi, ushirikiano na uwezo wa kifedha.

TBL inampango wa kuwasaidia wakulima kuongeza uzalishaji kwa kutumia rasilimali asilia hasa wakulima wa kilimo cha Mtama. Shayiri na zabibu.Ambazo ni rasilimali muhimu kwa shughuli za TBL, mpango huu unawasaidia wakulima moja kwa moja katika kuongeza uzalishaji na kutumia rasilimali asilia kwa ufanisi.

Akizungumza kuhusu ushirikiano huo Michelle Kilpin ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Breweries Limited, amesema: "Kwa kuunganisha juhudi za TBL na CRDB Bank Foundation, ushirikiano utasaidia kuongeza ukuaji wa sekta ya shayiri na kuimarisha ustawi wa kiuchumi wa wakulima wadogo wadogo nchini Tanzania.

“ Ninaamini kuwa ushirikiano wetu ni mfano mzuri wa jinsi ushirikiano unavyoweza kuchangia mabadiliko chanya na kuunda thamani kwa wadau mbalimbali. Tukiwa tumefikia hatua hii leo, tuna imani kuwa itakuwa chachu ya shughuli kama hizo kote nchini, na tunaamini kuwa mpango huu utakuwa chanzo cha hamasa kwa wengine."

Kupitia muungano huo na CRDB Bank Foundation, TBL inalenga kuunganisha vigezo vya uwezeshaji wa kifedha kupiti mnyororo wake wa kilimo ili kuwawezesha wakulima kujihusisha na kilimo endelevu, kinacho chochea utunzaji wa mazingira na kupunguza kutegemea kwa kemikali za kilimo.

Amesema ushirikiano huo unathibitisha ahadi ya TBL ya kufikia Malengo Endelevu ya Umoja wa Mataifa, haswa SDG 2, SDG 12, SDG 13, SDG 17 huku akisisitiza pia ushirikiano wa Tanzania Breweries na CRDB Bank Foundation unalenga kuwezesha ukuaji endelevu wa wakulima wadogo wadogo.

Mpango wa CRDB foundation, uitwao iMbeju, unalenga kuimarisha sekta ya shayiri na kuongeza ustawi wa kiuchumi wa wakulima wadogo wadogo katika Wilaya za Manyara, Karatu, na Monduli kwa msimu wa kilimo wa 2024. TBL na CRDB Bank Foundation wanakusudia kukuza uimara na uthabiti wa muda mrefu katika sekta ya kilimo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, Bi Tully Esther Mwambapa, anasema programu ya iMbeju imekuwa sokoni kwa karibu mwaka mmoja sasa na imevutia idadi kubwa ya vijana na wanawake.

Ameongeza mpaka sasa programu hiyo, ambayo inajumuisha mafunzo ya elimu ya kifedha na utoaji wa mtaji wa mbegu, imewafundisha wanawake takriban 250,000 na kuwapa mtaji wa mbegu kiasi cha Sh.bilioni 5.

"Tunatafuta kuboresha kilimo endelevu kwa kuwawezesha wakulima wetu kifedha. Mara tu wakulima watakapokuwa na uhakika wa kifedha, uzalishaji utaongezeka zaidi katika mazao muhimu yote, kuimarisha usalama wa chakula chetu, na kuongeza ziada kwa biashara na usafirishaji wa ndani. Hii itakuwa na athari chanya kwa Pato la Taifa letu, ambapo kilimo kinachangia sehemu kubwa," ansema Bi. Tully.

Amefafanua chini ya ushirikiano huo, wakulima watapata ufikiaji wa pembejeo za kilimo kwa wakati unaofaa, na watapokea mafunzo kamili, yote ambayo yataongeza mavuno na kuboresha mapato kwa familia za wakulima. Zaidi ya hayo, juhudi hizi zitasaidia ukuaji wa kiuchumi na ustawi wa jamii hapa nchini

Kupitia ushirikiano huu, TBL na CRDB Bank Foundation watatoa programu za kuimarisha uwezo, mtaji wa mbegu, bima, usambazaji wa pembejeo muhimu za kilimo kama mbolea na dawa za kilimo, na msaada kwa mikakati ya mavuno.
 

Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Foundation, Tully Esther Mwambapa (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Michelle Kilpin wakitiliana saini mkataba huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...