WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Timu ya Mawaziri itakwenda wilaya za Rufiji na Kibiti mkoani Pwani kuungana na timu ya watalaam ili kufanya tathmini ya pamoja kutokana na athari zilizosababishwa na mafuriko yaliyotokea wilayani humo.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumanne Aprili 09, 2024) wakati wa hafla ya Futari aliyoiandaa kwa ajili ya watumishi wa ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zake, Mlimwa jijini Dodoma.

“Sisi ndio tunaratibu Idara ya Maafa kitaifa, hapa tunapozungumza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Jenista Mhagama pamoja na Katibu Mkuu Dkt. Jim Yonaz wako njiani wanaelekea mkoani Pwani, mto rufiji umejaa na kata nne zipo kwenye maji, Mawaziri wengine wa Sekta ikiwemo Afya, Kilimo, Mifugo nao pia wanakwenda ili kuimarisha uratibu wa zoezi”

Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Waziri Mkuu ameipongeza Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya namna inavyodhibiti biashara ya dawa za kulevya nchini.

“Kamishna amefanya kazi nzuri na kuboresha kwenye sekta yake, hivi sasa Taasisi yake haiishii tu Makao Makuu ya nchi, ameshusha kwenye kanda na tayari wakurugenzi wameshaenda kwenye maeneo hayo ambao watakamata wazalishaji, wasafirishaji, wafanyabiashara na watumiaji wa dawa za kulevya”

Viongozi wengine walioshiriki katika iftar hiyo ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Deogratius Ndejembi, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Ummy Nderiananga, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mary Maganga na Wakuu wa Taasisi zilizochini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...