Dar es salaam.

Ujumbe kutoka Asasi ya Umoja wa Kimataifa wa Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia (EITI) ukiongozwa Katibu Mtendaji Bw. Mark Robinson na umekutana na wawakilishi wa Kampuni za Madini na Gesi na mashirika ya Umma ya TPDC na Stamico kujadili utekelezaji wa shughuli za EITI nchini.

Maeneo yaliyolengwa katika majadiliano hayo ni ushiriki wa kampuni na mashirika ya Umma (State Owned Enterprises -SOEs) yanayofanya shughuli za Uziduaji katika utekelezaji wa vigezo vya Kimataifa vya Uwazi na Uwajibikaji vya mwaka 2023 ( EITI Standard 2023) Aprili 4, 2024 jijini Dar es Salaam.

Mapitio ya matokeo ya Tathmini (Validation) ya mwaka 2023 ambapo masuala yafuatayo yalipendekezwa kuboreshwa ili Tanzania ifanye vizuri katika Tathmini ijayo ya mwaka 2027, uwekaji wazi wa mikataba ya Madini na Gesi Asilia na uwekaji wazi wa Wamiliki wanufaika (Beneficial Owners) katika kampuni za Madini, Mafuta na Gesi Asilia.

Mchango wa wachimbaji wadogo na urasimishaji wa sekta ya uchimbaji mdogo.

Ushiriki wa kampuni na SOEs katika utekelezaji wa vigezo vipya vilivyoongezwa (EITI Standard 2023). Vigezo hivyo ni pamoja na masuala ya kuzuia rusha, jinsia na mazingira na Energy Transition.

Aidha, katika majadiliano hayo, ilielezwa kuwa baadhi ya kampuni tayari zimeweka wazi mikataba yake kupitia masoko ya hisa na hivyo iko wazi kwa Umma pia ilielezwa kuwa uwekaji wazi tayari mikataba utasaidia kuhamasisha Uwazi na wananchi kujua faida kutoka katika uvunaji wa rasilimali madini Mafuta na Gesi. Wawakilishi watatoa ushirikiano kwa Sekretariati ya EITI Tanzania katika utekelezaji wa vigezo vya Kimataifa vya mwaka 2023.

Pia, Wawakilishi wa kampuni na mashirika yafuatayo walihudhuria. Pan Africa Energy, Maurel & Prom, Tanzania Chamber of Mines, Tembo Nickel, Shanta Gold Mine, TPDC na Stamico.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...