Na John Walter -Manyara

Wafanyakazi wameiomba serikali kushughulikia changamoto waliyonayo kwa muda mrefu juu ya kikokotoo cha mafao pindi wanapostaafu.

Akizungumza katika maadhimisho ya Meimosi yaliyoandaliwa na shirikisho la vyama la Wafanyakazi (TUCTA) mkoa wa Manyara yaliyofanyika April 29,2024 uwanja wa Tanzanite Kwaraa mjini Babati , Katibu wa TUICO mkoa wa Manyara Juma Makanyaga amesema hawaridhishwi na kikotoo kilichopo cha asilimia 33.3 kwani kimekuwa ni mateso kwa watumishi na kupelekea sintofahamu kubwa kwa wafanyakazi na mustakabali wa maisha yao.

Wamemuomba Rais Samia Suluhu Hassan alitazame jambo hilo kwa jicho la tatu kwani kinachotumika hakiakisi hali halisi ya wanachama na kupendekeza kifanyiwe mabadiliko au kirudishwe kikotoo cha asilimia 50 ili kukidhi matakwa yao.

Katika hatua nyingine wameiomba serikali ifike Mahali ione umuhimu wa kuboresha mishahara kwa wafanyakazi wote.

Aidha wameiomba ofisi ya Katibu tawala mkoa wa Manyara kuishirikisha ofisi ya Shirikisho la Wafanyakazi katika shirikishwa masuala mbalimbali kwani ni muda mrefu serikali imeshindwa kufanya hivyo.

Kwa upande wake mgeni Rasmi mkuu wa wilaya ya Babati Lazaro Twange amesema amepokea maelekezo kutoka kwa katibu tawala mkoa kwamba Mei 3,2024 atakutana na Wafanyakazi wote kwa ajili ya kuwasikiliza na kutatua changamoto zilizopo.

Kuhusu mishahara kupanda na kikotoo amewataka Wafanyakazi waendelee kuwa watulivu wakati huu serikali inapotafuta ufumbuzi na kwamba Mei mosi jijini Arusha atakapokuwa akihutubia Rais Samia Suluhu Hassan huenda akazungumza jambo.

Sherehe za Mei mosi mwaka huu kitaifa zinafanyika mkoani Arusha na mgeni Rasmi atakuwa Samia Suluhu Hassan Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kauli mbiu ya Mei mosi 2024 “Nyongeza ya Mishahara ni Msingi wa Mafao Bora na Kinga Dhidi ya Hali Ngumu ya Maisha”




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...