Na Mwamvua Mwinyi,Pwani April 5
.jpeg)
Mchatta aliyasema hayo wakati akikabidhi vyeti vya kwa wajasiriamali wenye viwanda vidogo na vidogo kabisa wa mkoa huo ambao wametambuliwa na Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO) Mkoa wa Pwani.
Alisema kuwa wajasiamali hao wanapaswa kuzingatia ubora na viwango pia kushirikiana na taasisi zinazothibitisha viwango vya bidhaa ili ipate soko ndani na nje ya nchi.
Aidha aliipongeza SIDO kwa jitihada za kuwawezesha wajasiriamali ambapo Mkoa huo una jumla ya viwanda 1,533 vikubwa 122 vya kati 120 vidogo 274 na vidogo sana 1,117.
Naye Meneja wa SIDO Mkoa wa Pwani Beata Minga alisema ,mkoa unatambua jitihada za wajasiriamali ambao wameanzisha viwanda ambavyo vitaongeza ajira na kuongeza pato la mwananchi mkoa na Taifa.
Minga alifafanua, vyeti hivyo vya kuwatambua vitawasaidia pale wanapohitaji kutambuliwa na taasisi nyingine ambazo ni za uwezeshaji .
Zoezi hilo litakuwa endelevu ambapo jumla ya wajasiriamali 65 wametambuliwa.
.jpeg)


Minga alifafanua, vyeti hivyo vya kuwatambua vitawasaidia pale wanapohitaji kutambuliwa na taasisi nyingine ambazo ni za uwezeshaji .
Zoezi hilo litakuwa endelevu ambapo jumla ya wajasiriamali 65 wametambuliwa.
.jpeg)


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...