NA EMMANUEL MBATILO,MICHUZI TV

WADAU mbalimbali wa masuala ya Jinsia na Maendeleo wamekutana katika Semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS) na kuichambua bajeti ya Ofisi ya Rais (Mipango na uwekeshaji) na kubaini kuwa haijazingatia masuala ya jinsia.

Akizungumza leo Aprili 24,2024 jijini Dar es salaam, wakati wa semina ambazo hufanyika kila Jumatano katika Ofisi za TGNP Mtandao, Mhadhiri Chuo Kikuu Mzumbe Lihoya Chamwali amesema uwekezaji ambao umekuwa unafanyika kwa wanawake haukuzingatiwa hasa kufufua viwanda ambavyo wanawake wamekuwa wakishiriki.

Aidha ameishauri serikali kutoa elimu kwa wananchi kuhusu maswala ya uwekezaji kwani elimu hiyo imekuwa haijulikani kwa watu wengi hasa wanawake.

"Tunaishauri serikali iweke mifumo rafiki na elimu itolewe ili kila mwanamke ambae anaweza kuwekeza aweze kuingia kwenye mfumo na ndio maana tunasisitiza elimu itolewe kwani mifumo mingi ya uwekezaji inafanyika kielektroniki kitu ambacho wanawake wanawake wamekuwa wanaachwa kwa sababu wengi hawana ujuzi wa elimu hiyo". Amesema Chamwali.

Amesema bajeti ya mwaka huu imekuwa ndogo tofauti ya mwaka jana kwani mwaka 2023 bajeti ilikuwa bilioni30 lakini mwaka huu bilioni 17.

Amesema kufuatia na upungufu huo wa bajeti katika kupitia malengo wameona malengo mengi ya mwaka huu ni muendelezo wa malengo yaliyofanyika mwaka jana ikiwemo kupitia uundaji wa sera ya dira ya maendeleo 2050.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kituo cha maarifa kata ya Majohe Tabu Ally ametoa rai kwa serikali kuwaangali wanawake waliopembezoni ili waweze kujikwamua kiuchumi kwa kuwapa elimu bora ya uwekezaji.

Amesema changamoto kubwa inayowakabili wanawake waliopembezoni ni miundombinu ya barabara kwani wanazalisha lakini wanashindwa kufika sokoni kutokana na uharibifu mkubwa wa barabara hivyo inawalazimu kutumia ghalama kubwa ili kufika sokoni jambo ambalo linawarudisha nyuma kimaendeleo.

"Kila kitu ili kiende ni lazima barabara zipitike na hiyo ndio changamoto ambayo sisi tunalia nayo lakini hata tukiwezeshwa mitaji bado tutashindwa kutokana na hii moundombinu",Amesema Tabu

Naye,Mdau wa maswala ya jinsia kutoka Kigamboni Ayub Sharif amesema serikali inapaswa kutoa kipaumbele kwenye maeneo ambayo nguvu kazi kubwa inatumika ili kuongeza motisha ya ufanyaji kazi.

"Mimi naishauri serikali kuangali maeneo ambayo nguvukazi kubwa inatumia ndio uwezeshaji uanzie kwani tumeona katika sekta ya madini wanawake ndio wachenjuaji wakubwa lakini madini yakipatikana anaenufaika mwingine hii sio sawa serikali inapaswa kuangali swala hili kabla ya kuwekeza kwenye mitambo waweke mazingira mazuri kwa hizi nguvu kazi". Amesema.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...