Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb) amekutana na Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo na Mabadiliko ya Tabianchi wa Denmark, Mhe. Dan Jørgensen ambapo nchi hizi mbili zimeangazia maeneo ya ushirikiano na kukubaliana kuongeza ushirikiano kwenye sekta za kimaendeleo.

Tanzania na Denmark zinaenda kuongeza ushirikiano kwenye maeneo ya biashara, miundombinu, umeme, uwekezaji, kubadilishana uzoefu kwenye teknolojia pamoja na nishati safi na salama ikiwa ni sehemu ya kutunza mazingira na tabianchi kwa manufaa ya jamii ya sasa na baadaye.

Pande zote mbili zimeonesha kufurahishwa na mwelekeo wa ushirikiano huu ambapo Denmark ilionesha dhamira hiyo kwa vitendo mwaka 2023 baada kutengua uamuzi wake wa kuufunga ubalozi wake nchini.

Waziri Jørgensen yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili inayotarajiwa kufikia tamati hapo kesho.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...