Na Mwandishi wetu, Arusha

KAMPUNI ya Barrick nchini, imedhamini na kushiriki katika kongamano la wanafunzi wa vyuo vikuu lililoandaliwa na taasisi ya kuchipua na kuendeleza vipaji vya uongozi kwa vijana (AIESEC Tanzania) lililofanyika katika Chuo cha Uhasibu cha Arusha na kuwashirikisha wanafunzi, wahadhiri na wadau mbalimbali.

Kupitia kongamano hilo ambalo hufanyika kila mwaka, wanafunzi huweza kufahamu jinsi taasisi mbalimbali nchini zinavyoendesha shughuli zake lengo kubwa likiwa ni kuwajengea uwezo wa kujua vipaji walivyonavyo, kujifunza jinsi ya kujiamini na kukabiliana na ushindani katika soko la ajira, kujitambua uwezo wao ni jinsi gani wanaweza kushiriki kutoa mchango wa kuendeleza taifa pindi wamalizapo masomo yao.

Maofisa Rasilimali Watu Waandamizi wa Barrick pia walishiriki katika maonesho na kongamano hilo ambapo walipata fursa ya kuzungumza na wanafunzi kuhusiana na kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo ajira,kuendeleza vipaji vyao pia wanafunzi walipata fursa kuelewa jinsi kampuni ya kimataifa ya Barrick, inavyoendesha shuguli zake kwa kutoa kipaumbele kusaidia jamii sambamba na mpango wake wa kuibua na ukuzaji wa vipaji kwa vijana wa kitanzania na wafanyakazi wake.
Mwisho

Makamu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha, Profesa Ephraim akiongea katika kongamano la wanafunzi lililoandaliwa Taasisi ya AIESEC.
 

Afisa Raslimali Mwandamizi wa Barrick North Mara, Daniel Paul akiongea na wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu mkoani Arusha katika kongamano la wanafunzi lililoandaliwa na taasisi ya AISEC na kufanyika katika chuo cha Uhasibu cha Arusha kwa udhamini wa kampuni ya Barrick.
Wanafunzi wakifuatilia mada katika kongamano hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...