Na. Saidina Msangi, WF, Dodoma.

Serikali imesema kuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imetoa leseni kwa kampuni mbili za kuchakata taarifa za mikopo, kampuni hizo ni Creditinfo Tanzania Limited na Dun & Bradstreet Credit Bureau Tanzania Limited.

Hayo yameelezwa bungeni, jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Martha Nehemia Gwau, aliyetaka kujua idadi ya Kampuni za kutoa Taarifa za Mikopo (Credit Reporting Company) zinazoangalia hali ya kifedha ya mkopaji na uwezo wake wa kulipa hapa nchini.

Mhe. Chande alisema kuwa Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006, imeipa Benki Kuu mamlaka ya kuanzisha na kusimamia kanzidata ya taarifa za wakopaji (credit reference system), kutoa leseni na kusimamia kampuni binafsi za kuchakata taarifa za mikopo (Credit Reference Bureaux).

‘‘Taasisi zote za fedha kubwa na ndogo zinatakiwa kupeleke taarifa sahihi Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambayo inasimamia kanzidata ya taarifa za wakopaji na kila baada ya mwezi taarifa hizo zinapokelewa na kusambazwa katika taasisi zinazohusika’’, alifafanua Mhe. Chande.
 

 Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), akijibu swali bungeni jijini Dodoma.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Fedha)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...