Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imetambulisha rasmi huduma yake ya kidigitali ya ‘NBC Connect’ Visiwani Zanzibar. Huduma hiyo ya kisasa mahususi kwa makampuni pamoja na taasisi mbalimbali huwezesha huduma salama na haraka za kibenki kwa njia ya mtandao ikiwa ni muitikio wa benki hiyo katika kuunga mkono jitihada za serikali za kuongeza ujumuifu katika huduma za kifedha (financial inclusion).

Hafla ya utambulisho wa huduma hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki Zanzibar ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi-Zanzibar, Dkt. Mngereza Mzee Miraji. Hafla hiyo pia ilihusisha uwepo wa wateja wa benki hiyo visiwani humo, huku wafanyakazi wa benki hiyo wakiongozwa na  Mkuu wa kitengo cha wateja wakubwa na wateja wa serikali Benki ya NBC Linley Kapya.

Akizungumza kwenye tukio hilo lilidumu kwa siku tatu ambalo ni muendelezo kufuatia matukio kama hayo yaliyofanyika mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na Kanda ya Ziwa, Kapya alisema huduma hiyo ya kidigitali ni uthibitisho wa dhamira ya benki hiyo kuwapatia wateja wake huduma bora za kibenki ambazo ni rahisi, salama na zinazofaa na kukidhi mahitaji ya wateja.

“Kinachofanyika leo ni utambulisho rasmi wa huduma hii kwa kuwa tayari wateja wetu wameshaipokea huduma hii na wanaifurahia. Tupo hapa kupata mrejesho na kutoa ufafanuzi kwenye maeneo muhimu ili waweze kuifurahia huduma hii kwa upana wake. Ikitumika vizuri huduma hii, wateja wetu wenye makampuni na taasisi mbalimbali zilizopo visiwani Zanzibar watapata fursa na uwezo wa kufanya miamala yao ya kifedha kwa urahisi zaidi na kupata uzoefu mpya katika kupata huduma za kibenki.’’ Alisema.

Akiizungumzia huduma hiyo, Dkt. Mngereza alisema imesaidia kuleta mapinduzi mapya katika utoaji wa huduma za kibenki huku ikichochea kasi ya ukuaji uchumi kupitia urahishwaji wa malipo na ukusanyaji wa mapato mbalimbali yakiwemo ya serikali.

“Utambulisho wa huduma hii ya NBC Connect hapa Zanzibar unakwenda sambamba na dhamira ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi kupitia huduma bora za kifedha na uchumi jumuishi. Kupitia huduma hii mashirika na taasisi mbalimbali zitaweza kufanya malipo kwa wakati bila usumbufu na kwa kuwa ni rahisi kwa huduma hii kuwafikia walengwa kwa wingi wao basi pia  itachagia ukuaji wa uchumi…naomba sana mashirika, taasisi na kampuni mbalimbali hapa Zanzibar waipokee huduma hii,’’ alisema

Akifafanua zaidi kuhusu huduma hiyo Mkuu wa Miamala na Amana za Wateja Wakubwa wa NBC, Bw Jimmy Myalize alisema huduma hiyo inawapa wateja uwezo wa kufanya miamala kirahisi popote, wakati wowote ikiwemo kufanya malipo ya ndani na nje ya nchi, malipo ya serikali pamoja na malipo kwa mkupuo bila kutumia muda mrefu kwa kutumia tu simu au kompyuta.

“Wateja pia wataweza kupata taarifa za miamala waliyofanya popote pale walipo pasipo kulazimika kwenda benki. Huduma hii imetengenezwa kwa teknalojia ya kisasa na yenye usalama wa hali ya juu ambayo imezingatia na kutoa kipaumbele kwenye usiri wa taarifa za mteja. Ubunifu wa huduma hiyo huakikisha taarifa za kifedha za wateja zinalindwa wakati wote.’’ Aliongeza.

Aliongeza kuwa pamoja na huduma hiyo benki hiyo imejipanga kutoa usaidizi binafsi kwa wateja kupitia kituo chake cha huduma kwa wateja ambapo wataalamu wa huduma hiyo wamejipanga kuwasaidia wateja kulingana na mahitaji yao na kutoa mwongozo wa jinsi ya kutumia jukwaa hilo kwa ufanisi.

Meneja wa Huduma za Miamala wa Benki ya NBC Charles Ndendeje  akifafanua kuhusu huduma ya kidigitali ya ‘NBC Connect’  inayotolewa na benki hiyo mahususi kwa makampuni pamoja na taasisi mbalimbali  wakati wa hafla fupi ya utambulisho wa huduma hiyo kwa wateja wa benki ya NBC Zanzibar iliyofanyika mwishoni mwa wiki Zanzibar. Hafla hiyo iliongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi-Zanzibar, Dkt. Mngereza Mzee Miraji.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi-Zanzibar, Dkt. Mngereza Mzee Miraji (wa pili kushoto) akijadili jambo na maofisa  waandamizi wa benki ya NBC wakati wa hafla fupi ya utambulisho wa huduma ya kidigitali ya ‘NBC Connect’  inayotolewa na benki hiyo mahususi kwa makampuni pamoja na taasisi mbalimbali  iliyofanyika mwishoni mwa wiki Zanzibar. Kushoto ni  Mkuu wa kitengo cha wateja wakubwa na wateja wa serikali Benki ya NBC Linley Kapya, Meneja wa Benki hiyo tawi la Zanzibar Ramadhan Lesso (wa pili kulia) na Mkuu wa Miamala na Amana za Wateja Wakubwa wa NBC, Jimmy Myalize (Kulia) 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi-Zanzibar, Dkt. Mngereza Mzee Miraji (pichani) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla fupi ya utambulisho wa huduma ya kidigitali ya ‘NBC Connect’  inayotolewa na benki ya NBC mahususi kwa makampuni pamoja na taasisi mbalimbali  iliyofanyika mwishoni mwa wiki Zanzibar.

Mkuu wa kitengo cha wateja wakubwa na wateja wa serikali Benki ya NBC Linley Kapya (pichani) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla fupi ya utambulisho wa huduma ya kidigitali ya ‘NBC Connect’  inayotolewa na benki ya NBC mahususi kwa makampuni pamoja na taasisi mbalimbali  iliyofanyika mwishoni mwa wiki Zanzibar.

Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Zanzibar Ramadhan Lesso (Pichani) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla fupi ya utambulisho wa huduma ya kidigitali ya ‘NBC Connect’  inayotolewa na benki ya NBC mahususi kwa makampuni pamoja na taasisi mbalimbali  iliyofanyika mwishoni mwa wiki Zanzibar.

Mkuu wa Miamala na Amana za Wateja Wakubwa wa NBC, Jimmy Myalize (pichani) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla fupi ya utambulisho wa huduma ya kidigitali ya ‘NBC Connect’  inayotolewa na benki ya NBC mahususi kwa makampuni pamoja na taasisi mbalimbali  iliyofanyika mwishoni mwa wiki Zanzibar.


Baadhi ya wateja wa benki ya NBC pamoja na maofisa wa benki hiyo wakifuatilia utambulisho wa huduma ya kidigitali ya ‘NBC Connect’  inayotolewa na benki ya NBC mahususi kwa makampuni pamoja na taasisi mbalimbali  ulofanyika mwishoni mwa wiki Zanzibar.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi-Zanzibar, Dkt. Mngereza Mzee Miraji (katikati -walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi pamoja na wateja wa benki ya NBC wakati wa hafla fupi ya utambulisho wa huduma ya kidigitali ya ‘NBC Connect’  inayotolewa na benki ya NBC mahususi kwa makampuni pamoja na taasisi mbalimbali  iliyofanyika mwishoni mwa wiki Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...