Na Elizabeth Msagula Lindi,

Katika kuhakikisha halmashauri ya manispaa ya Lindi inaongeza mapato,wananchi kunufaika kiuchumi na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi baraza la Madiwani Halmashauri ya Manispaa hiyo limepitisha mkataba wa makubaliano ya biashara ya hewa ukaa katika vijiji 10 , jumuiya za uhifadhi wa Misitu 3 na msitu wa hifadhi wa Manispaa na kampuni ya village climate solution limited (VCSL).

Wamepitisha mkataba huo katika kikao cha robo ya tatu ya baraza hilo wakieleza matumaini yao juu ya uwepo wa biashara hiyo kuwa itakuwa chanzo kipya cha mapato kwa Vijiji, Jumuiya za uhifadhi na halmashauri na kwamba mradi utakuwa na manufaa na kwa wananchi kwa ujumla.

Meneja Msaidizi wa Mradi huo Yahya Mtonda amesema Mradi huo utatekelezwa kwa kipindi kisichopungua miaka 40 katika Vijiji vya Kiwawa, Mputwa, Milola Magharibi, Ruhoma, Mkombamosi, Namkongo, Muungano, Kinyope, Likwaya, na Makumba.

Pia Sambamba na vijiji hivyo mkataba huu umehusisha jumuiya za uhifadhi wa misitu mitatu (3) ambazo zimeanzishwa pembezoni mwa mtaa wa Nandambi, pamoja na msitu wa hifadhi wa Makangara katika Manispaa hiyo ya Lindi nao pia umeingia katika Biashara ya hewa ukaa.

Amesema miongoni mwa sababu ya mradi huo kutekelezwa kwa miaka 40 ni kufanya ulizi wa Misitu hiyo kwa muda mrefu ili kupunguza hewa ukaa kwa kuhifadi Misitu hiyo ili viweze kuwasaidia vizazi vya sasa na vijavyo.

" kiasili misitu inaweza kuishi kwa muda mrefu hivyo basi kutokana na sababu hiyo basi miti inaweza kuendelea kuruhusu kufanyika kwa biashara hii ya hewa ukaa kwa kipindi hiko cha miaka 40”Alisema Mtonda

Aidha,ameeleza kwamba endapo mradi huo utakwenda vizuri malipo ya fedha zinazotokana na biashara ya hewa ukaa kwa kipindi cha miaka 40 zitaenda kwenye shughuli mbalimbali za vijiji vilivyopo kwenye mradi na hivyo kupata maendeleo makubwa.

Pamoja na kupitisha makubaliano ya biashara hiyo baraza hilo pia limepitisha mipango na sheria ndogo za uhifadhi wa Misitu kwa kijiji cha Milola, Mputwa na kijiji cha Namtamba baada ya kusaidiwa na shirika la kuhifadhi misitu Tanzania TFCG kuanzisha misitu ya hifadhi kwa kufanya matumizi bora ya ardhi ya vijiji vyao kwa kipindi cha miaka 40.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...