Na Janeth Raphael -MichuziTv

Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Kanda ya kati inayojumuisha mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora na Kigoma imefanya operesheni kwa kushirikiana na jeshi la polisi katika Wilaya ya Chamwino pamoja na Dodoma mjini, katika Wilaya ya Chamwino kata ya Sigala kijiji cha Izava pamoja na Dodoma Mjini Mamlaka imeteketeza ekari 9.5 za mashamba ya bangi na kukamata kilogram156. 23 za bangi na misokoto 127 watu 16 wamekamatwa na wanasubiri taratibu za kisheria kupelekea mahakamani.

Kamishina Msaidizi Kanda ya kati Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Mzee Kasuwi ameyabainisha hayo leo jijini Dodoma ambapo amesema katika operesheni hiyo watuhumiwa 2 wenye silaha za moto wamekamatwa na wanasubiri kupelekwa mahakamani.

"Watuhumiwa hao tumewakuta wakitumia silaha hizo kulinda mashamba ya bangi hivyo nikaona ipo haja ya kumuita mwenye mamlaka kisheria ya wahalifu waliokutwa na silaha kinyume cha sheria ambaye ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma na nimkabidhi silaha hizi"

Hata hivyo Kamishina Kasuwi ametoa wito na kuwaomba wananchi wote kutoa taarifa za watu wanaojihusisha na dawa za kulevya wapige simu namba 119.


Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Theopista Mallya amesema watu wote wanaojihusisha na kuuza, kununua na wanaotumia dawa za kulevya watakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

"Kwa Dodoma hapa matumizi ya bangi ni mengi na kuna maeneo ambayo tumeshaelekezwa na tunafuatilia na tutawakamata"

Kamanda Mallya amesema swala la kilimo cha bangi sio siri ni shamba linaloonekana na watu wanaishi huko na ni lazima watoe taarifa ili kuweza kuponyesha watumiaji ambapo ni janga kubwa kwa vijana.

Kamanda Mallya amewataja watuhumiwa hao walikamatwa na silaha hizo Kuwa ni Hamis Chambo (46) ambaye ni mzugua na ni mkulima na mwingine ni Abilahi Juma (45) mkulimaMichuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...