NA. MWANDISHI WETU

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba 108 za waathirika wa maafa ya maporomoka ya mawe, tope na miti kutoka mlima Hanang’ yaliyotea Wilayani Hanang’ Mkoani Manyara mwishoni mwa mwaka Jana, 2023.

Dkt. Yonazi amefanya ziara hiyo mwishoni mwa wiki ambapo pamoja na mambo mengine amesisitiza uwekaji wa mifumo ya anwani za Makazi katika nyumba hizo zitakazoonesha namba za nyumba na vibao vyenye majina ya mitaa kurahisisha utambuzi wa makazi na wakazi husika ili kurahisisha ufikishaji wa huduma na bidhaa mahali stahiki na kuchagiza maendeleo kwa wananchi hao.

Dkt. Yonazi ametoa maagizo hayo ya kuweka anwani za makazi kwa kuzingatia umuhimu wake katika nyumba hizo zinazojengwa katika eneo la Gidagamowd lililopo katika Kitongoji cha Waret Wilayani Hanang mkoani humo.

Alisema kuwa Serikali imetenga eneo la ekari 100 ambapo jumla ya viwanja 269 vimepimwa ambapo kati ya hivyo, viwanja 226 ni makazi pekee, viwanja 26 ni makazi na biashara na viwanja 17 ni maeneo ya huduma za kijamii.

Aidha amewata wakandarasi kukamilika utekelezaji wa mradi husika kwa wakati na kuzingatia ubora unaotakiwa.

“Mradi ukamilike kwa wakati kama ilivyokubalika yaani ndani ya siku tisini na uendane na thamani ya fedha itakayotumika pamoja na hilo endeleeni kushirikiana na wenyeji wa eneo hili ili kuimarisha mahusiano na wazawa,” alisisitiza Dkt. Yonazi

Akizungumza kuhusu maendeleo ya mradi huo Kaimu Operesheni Kamanda Luteni Kanali Ashraf Hassan ameahidi kuhakikisha kuwa maelekezo yaliyotolewa na Dkt. Yonazi yanafuatwa ili ujenzi ukamilike kwa wakati.

Luteni Kanali Ashraf amemueleza Katibu Mkuu kuwa ujenzi huo wa nyumba 73 umefikia asilimia 40, na unajengwa kwa kuzingatia vigezo vya ubora uliokusudiwa na Serikali.

"Tumefurahi kutembelewa na Katibu Mkuu Dkt. Yonazi ambaye ameeleza kuridhishwa na maendeleo ya mradi, na sisi tunamuahidi kuwa ujenzi huu utakamilika kwa wakati lakini pia kwa kuzingatia viwango vya ubora vilivyoelekezwa" amesema Luteni Kanali Ashraf

Akieleza faida za mradi wa ujenzi amesema kuwa umesaidia kutoa ajira kwa wenyeji, biashara ndogondogo hasa za mama lishe, kukuza uchumi wa wakazi wa Katesh pamoja na kuimarisha mahusiano na wakazi wa maeneo hayo pamoja na uboreshwaji wa miundombinu ya barabara, maji na umeme katika maeneo ya mradi.

Disemba 3, 2023 Wilaya ya Hanang’ ilikubwa na maafa yaliyosababishwa na maporomoko ya tope, miti na mawe Wilayani yaliyouwa zaidi ya watu 80 huku mamia wengine wakiachwa bila makazi.Serikali iliratibu masuala yote ya menejimenti ya maafa ikiwa ni pamoja na hatua ya kurejesha hali ambapo kwa sasa zinajengwa nyumba 108 za waathirika wa maafa hayo, ambapo nyumba 73 zinajengwa na Serikali kwa kutumia SUMAJKT na zingine 35 zinajengwa na Chama cha Msalaba Mwenkundu (Tanzania Red Cross Society) kwa kushiriana na wadau mbalimbali ili kurejesha makazi kwa wananchi hao.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akiangalia moja ya nyumba zinazojengwa kwa ajili ya waathirika wa maafa ya Hanang’ katika eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hizo la Gidagamowd lililopo katika Kitongoji cha Waret Wilayani Hanang’ mkoani Manyara.


Muonekano wa baadhi ya nyumba zinazojengwa kwa ajili ya waathirika wa maafa yaliyotokea Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara, nyumba hizo zinajengwa eneo la Gidagamowd lililopo katika Kitongoji cha Waret wilayani humo.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi (mwenye shati la batiki) akizungumza jambo na Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji mkoa wa Manyara Bw. Faraja Ngerageza (wa pili kutoka kulia) wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba za waathirika wa maafa Hanang’ zinazojengwa katika eneo la Gidagamowd lililopo katika Kitongoji cha Waret Wilayani Hanang’ mkoani Manyara.


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akitoa maelekezo wakati akikagua moja ya shimo la choo lililojengwa katika nyumba mpya za waathirika wa maafa ya maporomoko ya tope, mawe na miti kutoka mlima Hanang’ katika eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hizo la Gidagamowd lililopo katika Kitongoji cha Waret Wilayani Hanang’ mkoani Manyara wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo.


Kaimu Msimamizi Mkuu wa mradi wa ujenzi kutoka SUMA JKT  Meja Boniface Kitambi akimuonesha michoro ya ramani ya ujenzi wa nyumba za waathirika wa maafa ya maporomoko ya tope, mawe na miti kutoka mlima Hanang’ Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi (mwenye shati la batiki) wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba hizo katika eneo la Gidagamowd lililopo katika Kitongoji cha Waret Wilayani Hanang’ mkoani Manyara.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...