Exim Bank imeshirikiana na Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania (TRCS) pamoja na Mpango wa Damu Salama Tanzania (NTBS) kupanda miti na kuendesha zoezi la uchangiaji damu katika maadhimisho ya Siku ya Msalaba Mwekundu Duniani yaliyofanyika jijini Dodoma ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Dkt Dotto Biteko, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati.

“Benki ya Exim tumejumuika pamoja hapa Dodoma kukumbuka na kuthamini kazi nzuri na ya muhimu inayofanywa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania (TRCS) kwa sababu tunatambua umuhimu wa kazi zake katika kusaidia jamii yetu, na tunaahidi kuendelea kuwa mshirika mwaminifu katika kuleta mabadiliko chanya,” anasema Stanley Kafu, Mkuu wa Kitengo cha Masoko kutoka Exim Bank.

Kupitia mpango wake wa kijamii unaoitwa ‘EXIM Cares’, Exim Bank ina miradi kadhaa ya kijamii na kimaendeleo ambayo imekuwa ikitekelezwa nchini Tanzania. Baadhi ya miradi hiyo ya benki ni katika sekta za afya, elimu, mazingira, ubunifu, na masuala ya kifedha.

Akielezea moja ya miradi hiyo, Stanley alisema, “Kupitia mradi wetu wa ‘EXIM Go Green’ tumeshirikiana na wadau kuiunga mkono serikali kutunza mazingira kwa kupanda miti. Mfano tumeshiriki kupanda miti katika kata ya Zuzu iliyopo hapa Dodoma tukiongozwa na Mhe. Mizengo Pinda, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia benki yetu imeshiriki kupanda miti katika Hospitali ya Rufaa ya hapa Dodoma na soko la Machinga Complex.”

Kwa upanda wa afya, Exim bank imekuwa ikishirikiana na Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania pamoja na Mpango wa Damu Salama Tanzania (NTBS) kusaidia katika zoezi la uchangiaji damu ikitambua umuhimu na uhitaji wake kwa Watanzania.

“Mwaka jana tulishirikiana na Mpango wa Damu Salama Tanzania (NTBS) kuratibu zoezi la uchangiaji damu katika mikoa ya Mbeya, Mtwara, Mwanza, Dar es Salaam na hapa Dodoma ambapo tulitambuliwa na Serikali kama moja ya wadau wakuu katika zoezi la uchangiaji damu hapa nchini,” anafafanua Stanley.

Mwaka huu, Exim bank imeendelea kushirikiana na Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania katika maadhimisho hayo yenye kaulimbiu ya "Natoa kwa furaha, na furaha ninayotoa ni zawadi." ikisisitiza umuhimu wa kujitoa ajili ya afya njema kwa wenye mahitaji na furaha inayoambatana na kitendo hicho kwa pande zote mbili kwa mtoaji na mpokeaji.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa benki ya EXIM, Stanley Kafu (aliyeshikilia kipaza sauti), akitoa maelezo kwa Dkt. Dotto Biteko, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati (wa tatu kutoka kushoto), kuhusu mipango ya EXIM alipotembelea banda la benki hiyo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Msalaba Mwekundu Duniani yaliyofanyika tarehe 11 Mwezi huu jijini Dodoma. Benki ya Exim kupitia mpango wake wa kijamii wa 'Exim Cares', imekuwa ikiunga mkono miradi mbalimbali katika sekta kama afya, mazingira, elimu, ubunifu, na masuala ya kifedha.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...