Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha Mei 9

MTOTO Angel Mseven (8) mwanafunzi wa darasa la pili shule ya msingi Carisa Mwendapole, Kibaha mkoani Pwani amekutwa amefariki dunia ndani ya shimo la maji taka.

Alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani, Pius Lutumo alisema, mnamo tarehe 7, Mei saa 3:15 asubuhi huko katika kituo cha polisi Kibaha, ilipokelewa taarifa ya mtoto kuzama maji kwenye shimo na kusababisha kifo chake.

Alieleza, mtoto huyo ilisemekana alikuwa anacheza na watoto wenzake eneo hilo na baadae kukutwa tayari amefariki.

Lutumo alifafanua, uchunguzi wa awali wa Jeshi la Polisi mkoa kwa kushirikiana na vyombo vingine vya kiuchunguzi umebaini kwamba mtoto huyo aliuawawa kisha kisha kutumbukizwa katika shimo hilo tofauti na taarifa iliyopokelewa awali.

Lutumo alieleza, Jeshi la Polisi mkoa limeshaanza msako mkali wa kuwatafuta watu ama mtu aliyehusika na tukio hilo.

Jeshi hilo limetoa wito kwa raia wema wenye taarifa sahihi ya tukio hilo kujitokeza kutoa ushirikiano wa kufanikisha kuwakamata wahusika haraka iwezekanavyo ili haki iweze kutendeka.

Mnamo tarehe 6 Mei, Mwalimu Mseven wa shule ya sekondari Tumbi ilisambaa taarifa kwenye makundi mbalimbali ya watsapp kuwa amepotelewa na mtoto akiwa amevaa nguo ya kitenge ambapo baadae taarifa zilitolewa kwamba amepatikana lakini akiwa amefariki dunia.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...