Watuhumiwa Bharat Nathwani (katikati) na mke wake Sangita Bharat anayeshuka ngazi wakishuka ngazi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam ambapo kesi yenye mashtaka manne dhidi yao ikiwemo kumjeruhi jirani yao inasikilizwa.
Na Mwandishi Wetu
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa jinsi wanandoa Bharat Nathwan (57) na Sangita Bharat (54) walivyomshambulia jirani yao Lalit Ratilal na kutoa matusi ya nguoni kwa lugha ya kihindi.

Wanandoa hao ambao ni raia wa Tanzania wenye asili ya kihindi wanaoishi Mtaa wa Mrima - Kisutu, jengo la Lohana Dar es Salaam wanatuhumiwa kwa mashtaka manne likiwemo la kujeruhi mnamo Julai 21,2023 kinyume cha sheria.

Akitoa ushahidi wake, msimamizi wa Msikiti wa Wahindi Lohana, Ankit Dawda (32) mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Aaron Lyamuya amedai yeye anafanya kazi ya kusafisha mazingira ya msikiti, kupamba na kutoa mapambo pia kukusanya vitu vya msikiti huo, na kusimamia usafi na ukarabati jengo zima yenye nyumba za makaazi ambapo msikiti huo upo katika na jengo hilo.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Grace Mwanga akisiadiana na Frank Rimoy, shahidi huyo amedai, Julai 21,2023 akiwa ofisini kwake akiendelea na majukumu yake ya kazi, ghafla alifuatwa na watu ambao hakuwafahamu wakimueleza kwamba aende akaangalie juu ya ghorofa kuna makelele.

Amedai, alivyofika juu alikuta Sangita Bharat (mshtakiwa) akilalamika na kuwafokea mafundi waliokuwa wakifanya ujenzi katika eneo hilo watoe viroba vya vigae vilivyokuwa katika kibaraza wakati vitu vyote vilikuwa katika eneo la Lalit Ratilal (mlalamikaji) na hakuna kitu kilichopo katika eneo la lake.

Dawda anadai, kwa wakati huo kulikuwa na kelele nyingi zinaendelea, ndipo Sangita Bharat akaendelea kupaza sauti yake kwamba uchafu uliokuwa katika kibaraza chao utoke.

"Kwa sababu hao mafundi hawakutoa hivyo vigae, Sangita Bharat akaanza kurusha matusi kwa lugha ya kihindi, na hapo hapo waume zao wakawasilina Sangita akawa anaendelea kutoa matusi ambapo Kiran Lalit akapigwa na Bharat Nathwani (mshtakiwa, mume wa Sangita), hadi kuzamisha kichwa chake kwenye ndoo ya saruji akatumbukia huko na mume wake naye akapigwa kifuani, kichwani na mguuni akadondoka chini akazimia".

"Waliita ambulance wakamshusha chini wakapelekwa hospitali lakini sikujua ni hospitali gani wamepelekwa,"akadai

Awali, Fundi Seremala, Dominic Mpakani (43) aliileza mahakama jinsi mshitakiwa Bharat Nathwan allivyomshambulia jirani wake, Lalit Ratilal kwa kumpiga kichwa kifuani kisha akadondoka chini na nakupoteza fahamu kwa muda.

Aidha, alidai kuwa kulikuwa na ugomvi kati ya mke wa Bharat (Sangita Bharat) na mke wa Lalit, (Kiran) ambao walikuwa wakirushiana maneno kwa ukali kwa lugha ya kihindi huku, baada ya muda kidogo waume zao walifika kwa pamoja na kuingilia ugomvi huo.

Amedai kuwa Julai 21,2023 alikuwa nyumbani kwa Lalit Ratilal maeneo ya mtaa wa Mrima katika jingo la Lohana, alimuita kwa ajili ya kuifanyia kazi zinazohusiana na mbao na kazi zingine ndogo ndogo.

Amedai kuwa alifika katika jengo hilo saa tatu asubuhi ambapo bosi wake huyo anakaa floor ya tatu, wakati anaendelea na kazi alidai kuwa Sangita alikuwa amesimama kwenye dirisha lake na Kiran alikuwa amesimama kwenye mlango wake, kila mmoja alianza kuzungumza kwa ukali na kwa jaziba wakitumia lugha ya kihindi.

"Lakini nilimsikia mke wa Bharat, Sangita akimwambia mke wa Lalit kwamba uchafu wake apeleke huko ambapo vitu vyote vilikuwa vimewekwa katika eneo la Lalit na hakuna kitu chochote kilichokuwa katika eneo la Sangita. Baada ya dakika kadhaa sijui walipiga simu au vipi waume zao walikuja kwa wakati mmoja na malumbano yakaendelea kwa wote wanne," alidai Fundi Mpakani

Shahidi huyo amedai kuwa, wakati malumbano hayo yanaendelea wote walikuwa wamesimama kwenye mlango wa Lalit, baada ya muda Bharat akampiga kichwa Lalit na Lalit akadondoka chini na kupoteza fahamu.

Shahidi mwingine ambae ni Dkt. Lucia Augustino (52) wa Hospitali ya Mnanzi Mmoja alidai kuwa Julai 21,2023 alikuwa Idara ya Dharura chumba namba 20 muda wa mchana alipokea wateja wawili wenye asili ya kihashia walikuwa wamechafuka kuanzia kichwani hadi miguuni , mama alichafuka sana kuliko baba.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka inadaiwa, washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka manne ambapo, katika shitaka la kwanza la kujeruhi linalomkabili Nathwani peke yake, ambapo anatuhumiwa Julai 21,2023 akiwa eneo la mtaa wa Mrima-Kisutu, jingo la Lohana, ndani ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam kinyume cha sheria alimsababishia madhara makubwa Kiran Lalit kwa kuzamisha kichwa chake kwenye ndoo la saruji iliyochanganywa.

Pia, katika shitaka la pili la shambulio la mwili linalomkabili Nathwani peke yake, ambapo tarehe hiyo na eneo hilo alimsababishia madhara Lalit Ratilal katika mwili wake kwa kumpiga kichwa, ngumi na mateke kichwani.

Ilidaiwa kuwa katika shitaka la tatu na la nne linalomkabili Sangita peke yake, ambapo anatuhumiwa kutoa matusi makubwa dhidi ya Lalit na Kiran kitendo ambacho kilileta fujo kwa namna ambayo inaweza kuleta uvunjifu wa amani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...