Na; Mwandishi Wetu - Dodoma

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amekutana na Menejimenti ya Ofisi hiyo pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Ofisi hiyo kwa lengo la kujadili utekelezaji wa majukumu ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii katika Mwenendo wa ulipaji Mafao, Uwekezaji wa mifuko na tathmini ya uhai wa mifuko.

Kikao hicho kimefanyika leo Mei 4, 2024 kwenye ukumbi wa PSSSF, jijini Dodoma.

Aidha, Mheshimiwa Katambi ameitaka Mifuko ya Hifadhi ya jamii kuendelea kufanya uwekezaji wenye tija kwa wanachama sambamba na kuendelea kulipa mafao kwa wakati.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...