Say Raymond Mwakatundu (31) mkazi wa jijini Dar es Salaam amekamatwa na Polisi mkoani Njombe akiwa na fedha kiasi cha Milioni 29,374,000 katika nyumba ya kulala wageni (Guest) mjini Makambako fedha ambayo inadaiwa ameipata kwa njia ya wizi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Mahamoud Banga amesema walimkamata Mwakatundu wakiwa wanafanya upekuzi wa kawaida katika nyumba za kulala wageni ambapo baada ya mahojiano alikiri kuipata fedha hiyo kwa njia ya uporaji.

"Tulipofika katika nyumba ya kulala wageni ambayo inaitwa Lisbon ndio tulifanikiwa kumkamata akiwa na fedha hiyo lakini baada ya kumhoji kwa kina alieleza kwamba fedha hizo amezipora katika kampuni aliyokuwa anafanyia kazi ya Interchick Dar es Salaam"amesema Kamanda Banga

Aidha amesema tayari mtuhumiwa amekwishakabidhiwa kwa jeshi la Polisi mkoani Dar Es Salaam kwa ajili ya hatua zingine za kimashtaka ili aweze kufikishwa Mahakamani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...