Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof. Maulilio Kipanyula akizungumza wakati akifungua mafunzo ya viongozi wa Menejimenti na vikundi vya Watafiti yaliyoandaliwa na Taasisi hiyo kwa lengo la kuwajengea uwezo viongozi hao Mei 21, 2024 jijini Arusha.



Naibu Makamu Mkuu wa Taasisi Mipango,Fedha na Utawala Prof. Susan Augustino akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya viongozi wa Menejimenti na vikundi vya Watafiti yaliyoandaliwa na Taasisi hiyo kwa lengo la kuwajengea uwezo viongozi hao Mei 21, 2024 jijini Arusha.



Menejimenti na vikundi vya Watafiti kutoka Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyoandaliwa na Taasisi hiyo Mei 21, 2024 jijini Arusha.



Viongozi wa Menejimenti ya Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela wakila kiapo cha Uadilifu wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Menejimenti na vikundi vya Watafiti yaliyoandaliwa na Taasisi Mei 21, 2024 jijini Arusha.

.........

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof. Maulilio Kipanyula amesema uadilifu na kujitoa ni nguzo katika kutimiza majukumu ya uongozi na kujenga NM-AIST . Ameyasema hayo Mei 21, 2024 Arusha wakati akifungua mafunzo ya siku tano ya Menejimenti na Watafit yaliyoandaliwa na Taasisi hiyo kwa lengo la kuwajengea uwezo viongozi hao.

Mafunzo hayo yanalenga kuongeza uelewa wa uwajibikaji na uadilifu katika utumishi wa umma, miiko ya uongozi, usimamizi wa fedha za umma ,uandaaji wa bajeti , matumizi ya fedha kudhibiti na kusimamia msongo wa mawazo pamoja na kusimamia afya ya akili.

Mafunzo hayo ya maadili kwa watumishi wa umma yanatolewa na Katibu Msaidizi - Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Ndg.Gerald A. Mwaitebele.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...