





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo Maalum kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) Mhe. Moussa Faki Mahamat wakati wa Maadhimisho ya miaka 20 ya Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (AU) yaliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Amani na Usalama akimvalisha Nishani ya Heshima Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete kwa kutambua mchango wake katika eneo la Amani na Usalama Barani Afrika wakati wa Maadhimisho ya miaka 20 ya Baraza hilo. Maadhimisho hayo yalifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Amani na Usalama akimvalisha Nishani ya Heshima Rais Mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo kwa kutambua mchango wake katika eneo la Amani na Usalama Barani Afrika wakati wa Maadhimisho ya miaka 20 ya Baraza hilo. Maadhimisho hayo yalifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2024.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Amani na Usalama akimvalisha Nishani ya Heshima Rais Mstaafu wa Burundi Mhe. Domitien Ndayizeye kwa kutambua mchango wake katika eneo la Amani na Usalama Barani Afrika wakati wa Maadhimisho ya miaka 20 ya Baraza hilo. Maadhimisho hayo yalifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2024.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...