Leo tarehe 24.05.2024 Mh. Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Batilda Buriani amewataka wafanyabiashara kutoa ushirikiano wa kutosha kwa timu ya uelimishaji kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambayo inaendelea kutoa elimu ya kodi mlango kwa mlango kwa wafanyabiashara kwa kuwatembelea katika maeneo yao ya biashara.

Amewaomba wafanyabiashara wafunguke kwa TRA ili waweze kusikilizwa na kutatuliwa changamoto zao za kikodi pia amesisitiza matumizi sahihi ya risiti za EFD kwa wafanyabiashara kuhakikisha wanatoa risiti halali za EFD kila wanapofanya mauzo na wanunuzi kudai risiti sahihi kila wanapofanya manunuzi.

Ameyasema hayo alipotembelewa na timu ya uelimishaji ikiongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Elimu kwa mlipakodi na mawasiliano TRA Bw. Hudson Kamoga kwa lengo la kumpa maelezo juu ya zoezi zima la elimu kwa mlipakodi mlango kwa mlango na kliniki za kodi linaloendelea mkoani Tanga.

Aidha kwa upande wake Kamimu Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano TRA Bw. Hudson Kamoga amewaomba wafanyabiashara kutoa ushirikiano wakati wa zoezi hilo pia wenye changamoto zozote za kikodi na wanaohitaji huduma TRA wasisite kuhudhuria kliniki za kodi zitakazokuwa mtaani kwao kwa ajili ya kuwahudumia wafanyabiashara.

Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imekuwa ikiendesha kampeni ya elimu kwa mlipakodi mlango kwa mlango kwa kuwatembelea wafanyabiashara katika maeneo yao ya biashara na kuwapa elimu ya kodi. Kampeni hii imekuwa na manufaa makubwa kwa kuongeza ulipaji kodi wa hiari na sasa timu ya uelimishaji ipo Tanga kwa siku kumi 10 kuanzia tarehe 20.05.2024 ikitoa elimu ya kodi mlango kwa mlango na kuendesha kliniki za kodi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...