WASANII Washauriwa kutengeneza kazi zenye maudhui ya kiasili na kutumia lugha ya Kiswahili fasaha ili kuendelea Kutangaza lugha hiyo Kimataifa na kuvitangaza vivutio vilivyopo Tanzania zaidi.

Akizungumza na wadau wa sanaa nchini wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya "Kamatia Furushi" pamoja na chaneli mpya yenye maudhui ya Filamu,katuni kwa watoto "Swahili plus" ,St Toons,St Toonie,St Kids plus ,St Movies, Muwakilishi kutoka Bakita Edward Nnko amesema anatambua mchango mkubwa unaofanywa na kazi za filamu nchini katika kutangaza lugha ya Kiswahili na Kukipa thamani zaidi kwani kupitia kazi hizo mataifa mengine wamekuwa wakifatilia .

Kwa upande wake Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes David Malisa ameeleza kuwa wamekuwa wakitoa vipindi mbalimbali vyenye maudhui tofauti tofauti hivyo kwa sasa wamezindua chaneli mpya ambayo itawapa fursa zaidi wasanii wakitanzania kuonekana.

Aidha amesema Filamu zaidi ya 120 zitaonekana kupitia St Swahili plus ambapo Filamu hizo hazijawahi kuonekana popote pale zikiwa zimesheheni sura mpya (wasanii wachanga).

Pia amefafanua zaidi kuwa chaneli inapatikana katika kifurushi cha uhuru hivyo watazamaji wahakikishe vifurushi vyao vimelipiwa kwa wakati

Nae Msanii wa Filamu nchini Daudi Michael maarufu 'Duma ' amewapongeza Startimes kwa kuona ipo fursa ya kuwa wadau wakubwa wa kazi za Sanaa na kutengeneza daraja la wasanii kufanya vizuri na kutengeneza kazi zenye viwango na shindani.
 

Msanii wa Filamu nchini Daudi Michael maarufu kama Duma akizungumza machache kwa kutoa shukrani kwa Startimes kwa kuongeza nguvu kwa wasanii kwa kupokea kaz za wasanii hao kwa kuoneshwa chaneli mpya swahili plus ili wao waendelee kufanya kazi zenye ubora na zenye ushindani ili kulipa thamani soko la Kazi za Filamu nje na ndani ya nchi
 

Muwakilishi kutoka Baraza la Kiswahili (BAKITA) Edward Nnko akizungumza machache mara baada ya uzinduzi wa chaneli mpya zenye maudhui mbalimbali katika kisimbuzi cha Startimes na kuwataka wasanii kuendelea kuipa thamani Lugha ya Kiswahili na kuitangaza kupitia kazi za Filamu
 

Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes David Malisa akizungumza na Wanahabari na Wadau wa Filamu  wakati wa Uzinduzi wa chaneli mpya zenye maudhui mbalimbali ikiwemo Filamu,katuni na burudani St Swahili plus,St Toonie, St Kids na nyinginezo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...