Kikosi cha Timu ya Tabora United kesho kitashuka katika Uwanja wa Manungu Turiani mkoani Morogoro kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Soka Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa saa nane kamili mchana (8:00).

Nyuki hao wa Tabora ambao kwa sasa wanasimamiwa na Kaimu Kocha Mkuu Masoud Juma Irambona kiliwasili salama jana mkoani hapa na hivyo leo kitafanya mazoezi ya mwisho kabla ya mchezo huo.

Tabora United inafahamu kuwa mchezo wa kesho dhidi ya Mtibwa Sugar utakuwa na ushindani mkubwa kutokana na kwamba kila Timu haipo kwenye nafasi nzuri na hivyo kuhitaji kupata ushindi utakaowezesha kujinasua kushuka daraja moja kwa moja.

Tabora United itashuka kwenye mchezo huo ikiwa imetoka kupoteza mchezo dhidi ya Simba Mei 06 mwaka huu katika Uwanja wa Azam Complex Chamanzi na kwamba tayari makosa hayo yameshafanyiwa marekebisho kwenye uwanja wa mazoezi.

" Tunajua ugumu wa mchezo wa kesho ambao kimsingi kila mmoja anafahamu umuhimu wake, ukiangalia msimamo wa Ligi Tabora United tupo nafasi ya 15 tukiwa na alama 23, Mtibwa Sugar yupo nafasi ya 16 akiwa na alama 17, hivyo ni mchezo mgumu , lakini kwetu sisi tumefanya maandalizi na kwamba tupotayari kupambania Timu yetu iweze kubaki Ligi Kuu.

Hatuna wakati mzuri kwenye matokeo kiasi cha kwamba mashabiki wamekuwa na hofu juu ya kubaki kwenye Ligi Kuu ya NBC lakini niwatoe hofu kwamba bado tunanafasi ya kupambania ndoto za kila Mwanatabora kuona tunakuwa kwenye ramani hiyo msimu ujao.

Kwa upande wa Afya za wachezaji wote wapo vizuri, wanahari namorali kuelekea kwenye mchezo huo ambapo kila mmoja yupo tayari kutumika kwa ufanisi zaidi ili kufanikisha adhma ya kuendelea kubakia Ligi Kuu ya NBC soka Tanzania Bara.

Imetolewa leo Mei 08
Na Christina Mwagala
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Tabora United.
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...