Na WAF - Geneva, Uswisi

Serikali ya Jamhuri ya Muumgano wa Tanzania na Taasisi ya Global Fund kuendelea kushirikiana ili kutekeleza vipaumbele vya Serikali vinavyolenga kutokomeza magonjwa ya UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria.

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema hayo leo Mei 30, 2024 kwenye kikao na Mkuu wa Usimamizi wa Ruzuku wa Global Fund Bw. Mark Eldon-Edington kilichofanyika pembezoni mwa Mkutano wa 77 wa Shirika la Afya Dunia (WHO) Jijini Geneva nchini Uswisi.

"Nakushukuru sana Bw. Eldon-Edington kwa kuwa Taasisi yako ya Global Fund imechangia kwa kiasi kukubwa nchini Tanzania kupunguza vifo vitokanavyo na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria na pia kuimarisha mifumo ya afya iliyo stahimilivu na endelevu." Amesema Waziri Ummy

Aidha, Waziri Ummy amesema kwa sasa changamoto kubwa iliyopo katika Sekta ya Afya ni kutomudu ugharimiaji wa baadhi ya vipaumbele vya kukabiliana na magonjwa pamoja ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi ambayo yanaleta athari kubwa katika kutoa huduma za afya.

Kwa upande wake Bw. Eldon-Edington ameipongeza Tanzania kwa kupiga hatua kubwa katika kupunguza maambukizi mapya na vifo vitokanavyo na UKIMWI.

"Global Fund itaendelea kutoa kipaumbele kwa Tanzania katika kutoa msaada ili kuimarisha mifumo ya afya itakayowezesha uendelevu katika mwitikio wa kutokomeza magonjwa haya." Amesema Bw. Eldon-Edington






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...