NA BALTAZAR MASHAKA,MAGU

KITUO cha kulelea watoto wenye migongo wazi na vicwa vikubwa cha Nyumba ya Matumaini (Child Help Tanzania),kimepokea msaada wa vifaa mbalimbali vya sh. milioni Saba kutoka Taasisi ya The Desk & Chair Foundation.

Msaada huo vikiwemo viti mwendo,mashuka,vifaa vya elimu na kilimo cha umwagiliaji wa matone,ulitolewa na The Desk & Chair Foundation na kukabidhiwa kituoni hapo (Mei 12,2024)kwa watoto na watumishi wa kituo hicho.

Akikabidhi msaada huo leo, Mwenyekiti wa Taasisi hiyo,Dk.Alhaji Sibtain Meghjee,amesema msaada huo ni viti mwendo vitano,vyandarua 10,mashuka 40,vifaa saidizi vya walemavu 2,boksi tano za vifaa vya kilimo cha umwagiliaji ka njia ya matone.

Vifaa vingine ni boksi moja la sabuni za kuogea na miche ya kufulia pamoja na vifaa vya elimu (madaftari 100 na Counter books 10) kwa watoto wenye mgongo wazi na vichwa vikubwa wanaolelewa katika kituo cha Nyumba ya Matumaini cha Child Help Tanzania ( Kitongo Hope) .

“Tumetoa vifaa hivi viwasaidie watoto hawa wenye changamoto ya ulemavu wa migongo wazi na vichwa vikubwa wanaolelewa katika kituo cha Kitongo Hope,vinagharimu sh.milioni Saba,”amesema Dk.Alhaji Meghjee.

Meneja wa Kituo cha Nyumba ya Matumaini cha Kitongo Hope,Getrude Leizer amesema,msaada wa viti mwendo kwa watoto wenye changamoto ya ulemavu,vyandarua na mashuka vimekipeleka kituo hicho hatua kubwa na kuwaomba wadau wengine wajitokeze kuwasaidia watoto hao watimize ndoto zao.

Pia ameishukuru taasisi hiyo kuwaondolewa adha na changamoto ukosefu wa maji baada ya kuunganishwa katika mtandao wa maji wa mradi mkubwa wa kisima cha Kitongosima.

“Tulikuwa na changamoto ya ukosefu wa majisafi na salama kwa watumishi wa kituo na watoto pia,maji ya matumizi ya kilimo cha umwagiliaji wa bustani ya mboga mboga na matunda,”amesema Laizer.

Kwa upande wake mlezi wa watoto wa kituo hicho,Rechal Kakaya amesema hawakuwa na maji safi na salama ya kunywa na matumizi mingine,baada ya kuunganishwa katika mradi wa kisima sasa watoto watabadilisha mazingira ya shule.

“Niwashukuru The Desk & Chair Foundation kwa mradi wa maji,awali tulikuwa na changamoto kubwa sasa mazingira yatabadilika.Pia tunashukuru kwa vifaa vya elimu,umwagiliaji,vifaa saidizi kwa walemevu,elimu na viti mwendo, vyandarua, mashuka na sabuni kwa matumizi ya watoto Mungu awabariki sana,”amesema.

Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation, Dk.Alhaji Sibatain Meghjee (wa pili kulia),katika picha ya pamoja na watoto wenye ulemavu wa miguu, migongo wazi na vichwa vikubwa, leo baada ya kuwakabidhi viti mwendo vitano.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...