Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma

Timu ya Mpira wa Miguu Tanzania ya Simba leo May 17, 2023 imefanya zoezi la upandaji wa miti ikiwa inaelekea kwenye Mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya walima Zabibu Dodoma utakaochezwa leo hii kwenye Uwanja wa Jamhuri.

Katika zoezi hilo Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo Imani Kajula leo ameongozana na watendaji mbalimbali wa Klabu hiyo pamoja na mashabiki katika zoezi la upandaji miti kwa kushirikiana na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS)

Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa upandaji miti Kajula amesema kuwa uhai wa Nchi yetu unategemea Sana uwepo wa Misitu ya Kutosha na mazao yake, na wasiofamu wafahamu kuwa nyuki wote wa Tanzania wanahifadhiwa na TFS.

"Uhai wa nchi yetu unategemea sana uwepo wa misitu yakutosha na mazao yake, kwa wale wasiofahamu nj kwamba nyuki wote wa Tanzania wanahifadhiwa na TFS ndo mana tunasema bila nyuki hakuna uhai hayo yote niliyosema yanaonesha umuhimu wa Taasisi ya TFS kwa uhai wa nchi ya Tanzania ".

"Sisi kama klabu ya Mpira tunaamini kwenye maisha endelevu ikiwemo uwepo wa Misitu ya Kutosha na uhifadhi".

Aidha amesema kuwa klabu ya Simba inaamini katika Misitu.

"Leo hii tumeona tusitoke Dodoma bila kuacha kumbukumbu muhimu kwenye eneo la uhifadhi, kwenye Misitu ndipo ambapo Simba anapatikana,uhai utaendana Sana na uwepo wa Misitu"amesema

Akitoa salamu zake Kocha Mkuu wa Klabu hiyo ya Simba Juma Mgunda amewapongeza Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) kwa kuwashirikisha katika Jambo la upandaji miti na kuwahakikishia wapo pamoja.

Na kuongezamkuwa maka tunasema kuwa miti ni uhai basi jambo la upandaji miti ni lakwetu sisi viumbe tulio hai.

"Kama tunasema kuwa miti na misitu ni uhai basi jambo la upandaji miti ni la kwetu sisi viumbe tulio hai".

Kwa Upande wake Kamishna Msaidizi Mwandamizi na Meneja Rasilimali za Nyuki (TFS) Husein Msuya amesema kuwa kitendo walichokifanya Simba leo ni kuenzi Mazingira na kuenzi uwepo wa nyuki na viumbe hai wengine.

"Wiki hii pia tunaanza maadhimisho ya wiki ya siku ya nyuki duniani kwa ajili ya kusherehekea mchango wa nyuki kwenye Mazingira"amesema

Kwa upande wake Kamishna Msaidizi Mwandamizi na Meneja sehemu ya Bailojia ya mbegu (TFS) akimwakilisha Kamishna wa Uhifadhi Fandey Mashimba amesema kuwa huwa wanafurahi anapokuwepo Simba kwenye Msitu shughuli za binadamu hupungua kama ukataji wa miti na uharibifu mwengine wa Mazingira.

"Sisi TFS huwa tunafurahi kwenye misitu yetu akiwepo Simba kwasababu Simba akiwepo misitu huwa inakuwa salama shughuli za kibanadamu zinapungua uharibifu unapungua kwasababu uwepo wa Simba akiunguruma shughuli nyingi za kibinadamu zinapungua ikiwemo kilimo cha kuhama hama".

"Nakuomba Mtendaji wa Simba hiki kitendo cha upandaji miti kisiishie hapa tuendelee kupanda miti katika maeneo mbalimbali tunapopata nafasi na sisi TFS tupo kila Wilaya".

Upandaji wa miti ni moja kati ya Mambo Timu ya Simba waliyoyafanya hapa jijini Dodoma ambapo May 16,2024 walizindua Simba Executive Network wakati wakati wakisubiri Mchezo wao na Dodoma Jiji FC leo saa10:00.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...