TotalEnergies imeanzisha tena shindano lake la makampuni machanga ambapo inalenga kutoa tuzo kwa wajasiriamali 100 kutoka Afrika.

Shindano la mwaka huu, ambalo linajumuisha nchi 32 za Afrika ambapo kampuni hiyo inafanya kazi, limepewa "umuhimu maalum" wakati kampuni hiyo inasherehekea miaka 100.

Shindano hilo linayojulikana kama "Mwanzilishi wa Mwaka na TotalEnergies" inaingia mwaka wa nne sasa baada ya kufanya katika miaka iliyopita.

"Toleo hili jipya linaloanza leo linathibitisha tena dhamira ya TotalEnergies ya kukuza uvumbuzi na ujasiriamali na kusaidia maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya nchi za Afrika ambazo kampuni hiyo ipo," inasema taarifa ya kampuni hiyo. 

"Shindano hili linaimarisha ushirikiano ndani ya jamii kwa kusaidia wajasiriamali wenye uvumbuzi zaidi wa bara hilo kutekeleza miradi yao," iliongeza. 

Tangu kuanza kwa shindano hili mwaka 2015, washindi 365 - waliopatikana kutoka kati ya maombi zaidi ya 40,000 yaliyopokelewa - wamepewa tuzo na kusaidiwa ulimwenguni kote. 

Wakati wa shindano la 2021/2022 nchini Tanzania, TotalEnergies Marketing Tanzania iliwatambua wajasiriamali watatu vijana katika vikundi vya kampuni bora chini ya miaka mitatu, wazo bora la kuanzisha biashara, na mwanamke bora mjasiriamali. 

Katika shindano la mwaka huu 2024/2025, TotalEnergies itasaidia na kutoa tuzo kwa wajasiriamali vijana wenye umri kati ya miaka 18 hadi 35 wanaoishi Tanzania ambao wana mradi wa kuanzisha biashara au kampuni ya miaka mitatu au chini, katika sekta yoyote ya biashara. 

Jopo la majaji wa ndani litajumuisha wataalam, viongozi katika biashara, washiriki katika mfumo wa kampuni, wadau wa kudumu na wawakilishi kutoka TotalEnergies Marketing Tanzania watachagua washindi watatu katika makundi ya mjasiriamali bora, mradi bora unaozingatia uchumi, na mradi bora unaozingatia nishati endelevu na nafuu. 

Usajili wa makampuni utadumu hadi Juni 18, 2024 wakati maingizo yote ya miradi yatafanyiwa tathmini dhidi ya vigezo vinne: umuhimu kwa changamoto za maendeleo endelevu; uvumbuzi; uwezekano na uwezo wa maendeleo; na usawa wa kijinsia na ushirikishwaji wa wanawake katika mradi. 

Kila mshindi atapata zawadi ya fedha kiasi cha Sh20 milioni kwa mshindi na kampeni ya mawasiliano ya kuboresha uwazi wa mradi wao. Washindi pia watakuwa na fursa ya kukuza mradi wao wakati wa tukio hilo, maelezo ambayo yatatolewa baadaye. 

Mshindi wa shindano la Startupper msimu wa tatu la mwaka 2023, linaloendeshwa na kampuni ya TotalEnergies Marketing Tanzania Limited, Hellena Seilas (wa kwanza kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi shindano hilo lilivyomsaidia kufungua kiwanda cha kuchakata taka za plastiki hivyo kumwezesha kutunza mazingira ya maeneo pembezoni mwa fukwe za bahari. Pembeni yake ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Mamadou Ngom (katikati) na Mkuu wa Sheria, Mashirika, Rasilimali watu na Utawala wa kampuni hiyo Getrude Mpangile

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...