Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, ambaye pia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amewatembelea na kuwafariji wananchi waliothiriwa na mafuriko katika Kata za Kisiju na Shungubweni, Wilayani Mkuranga, mkoani Pwani.

Akitoa salamu za pole Mei 1, 2024, Mhe. Ulega amesema kuwa Mhe. Rais Samia amemtuma kuwafikishia wananchi hao salamu zake za pole pamoja na chakula, magodoro na vifaa vingine vya ndani ili viwasaidie katika kipindi hiki wakati serikali inaendelea kuchukua hatua za haraka kuhakikisha wananchi hao wanarejea katika maisha yao ya kawaida.

Sehemu kubwa ya wananchi hao ambao Mhe. Ulega amewatembelea nyumba zao zimeathiriwa kwa kuzingirwa na maji na kupelekea kukosa makazi na hivyo kulazimika kukaa katika makambi.

Jumla ya vitu ambavyo Mbunge huyo amekabidhi kwa niaba ya Mhe. Rais Samia ni Mchele tani 4, Unga tani 5 na Maharagwe tani 10 ambavyo amekabidhi kwa Vijiji vya Kerekese,Kalole,Mavunja na Kisiju pwani.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...