Na Mary Margwe, Simanjiro

Hali ya upatikanaji wa maji Vijijini katika Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara umefikia asilimia 66.7, huku kukiwa na aina 4 z vyanzo vya maji ikiwa ni pamoja na visima Virefu 76, Visima vifupi 15, mabwawa madogo 28, mabwawa ya kati/ makubwa 15.

Akizungumza wakati wa kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa RUWASA Kwa kipindi Cha robo ya tatu Januari -Machi kwenye baraza la Madiwani chini ya Mwenyekiti wake Mh Baraka Kanunga, Meneja wa RUWASA Wilaya hiyo Mhandisi Joanes Martine amesema taarifa hiyo ni ya miradi ya Maji Kwa kipindi Cha miezi hiyo mitatu.

Mhandisi Martine amesema Kwa Sasa Wilaya ya Simanjiro imefikia asilimia 66.7 ya upatikanaji wa maji Vijijini, ambapo pia kuna chemchem 12, na mto 1 ( Mto Ruvu ) ambazo ni Moja ya vyanzo vya maji Wilayani humo vyenye uwezo wa kuhudumia Wakazi wapatao 194,209.

"Katika kipindi Cha mwezi Januari -Machi 2024, Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilayanya Simanjiro Kwa kushirikiana na vyombo vya watoa hudumaya maji imefanya matengenezo ya visima ( Pampu ) vya maji katika Vijijini vya Lerumo, Kitwai B, Msitu wa Tembo, Okutu, matengenezo ya Genereta Kijiji cha Narakauo, Emboreet na matengenezo ya Mtandao wa mabomba katika Vijiji vya Engonongoi, Nyumba ya Mungu, Naisinyai na Lorkane" amesema Mhandisi Martine.

Aidha Mhandisi Martine amesema katika kipindi cha mwezi Januari - Machi ,2024 vyombo vya watoa huduma ya Maji ngazi ya jamii 16 vimeendelea kusimamia utoaji wa huduma ya Maji ya uhakika na utunzaji wa miradi iliyotekelezwa ili iwe endelevu.

" Hata hivyo kwa robo hii ya tatu tumefanikiwa kufanya Mafunzo na kikao kazi Kwa CBWSO's 11 na kuanza kutuma mifumo wa malipo ya kielektorikia ya Serikalini ( GePG ) amesema Meneja huyo.

Mhandisi Martine amefafanua kuwa Wilaya Ina jumla ya vituo 1851 vya kuchotea maji, kati ya hivyo vinavyofanya kazi ni 1627 ambapo kati ya hivyo vituo vya Umma ni 385, vituo vya majumbani ni 1,069, vituo vya Taasisi ni 135 pamoja na Mbauti ( Cattle trough ) za mifugo 38 zinazofanya kazi.

Aidha Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini ( RUWASA) Wilaya ya Simanjiro umeendelea na Utekelezaji wa Miradi ya Maji katika maeneo mbalimbali ya Wilayani hiyo huku Utekelezaji wake ukiwa katika hatua tofauti tofauti.

" Miradi 13 ni pamoja na mradi wa maji wa Olchoronyori, ukarabati wa miradi ya Maji Nyumba ya Mungu, ujenzi wa miradi wa maji Kijiji cha Nadonjukin, ujenzi wa mradi wa maji Kijiji cha Engonongoi, ujenzi wa mradi wa maji Kijiji cha Terrat , ufungaji wa mfumo wa Solar kwenye skimu 12 za maji katika Vijiji Emboreet, Naberera, losoito, Nadonjukin, Terrat, Ngage, Engonongoi, Langai, olchoronyori, Kambi ya chokaa, Narakauo na Nyumba ya Mungu kupitia program ya Carbon Credit " ameongeza Meneja wa RUWASA.

Amesema Usanifu wa miradi katika Vijiji vya Msitu wa Tembo, Kiruani , Londoto, Magadini , Korongo, Londrekes, Naberera, Okutu na Mwajanga.













Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...