Na Mary Margwe, Kaliua

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Mkoani Tabora Grace Quintine amesema wamefanya Kikao cha Ujirani mwema na Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua ili kupitia upya mipaka ya Kiutawala kati ya Wilaya ya Urambo na Kaliua kwa Maslahi mapana ya Wananchi ili kurahisisha huduma kikamilifu.

Quintine amesema kikao hiko kimehusisha kuwakutanisha viongozi mbalimbali wa Wilaya zote mbili wakiwemo wakulu wa Wilaya wakurugenzi pamoja na wataalam mbalimbali wakiwemo wa ardhi wa pande hizo mbili kwa lengo la kuweka usawa wa jambo hilo ili jamii iweze kuondokana na hali ya sintofahamu.

Amesema wakiwemo katika kikao hiko wamefanikiwa kujadili mambo muhimu kama ustawi wa Jamii kwani Wilaya ya Urambo na Kaliua ni majirani , hivyo basi wananchi wa Wilaya hizo mbili hushirikiana katika shughuli mbalimbali kama za kiuchumi ikiwepo biashara.

"Tumekutana hapa Kaliua kwa lengo moja la kuadili Mambo muhimu ikiwemo Ustawi wa Jamii kwani Wilaya ya Urambo na Kaliua ni Majirani hivyo basi Wananchi wa Wilaya hizi Mbili hushirikiana katika Shughuli za Kiuchumi ikiwemo biashara" amesema Mkurugenzi Mtendaji Grace

Aidha Quintine amesema kikao hiko kimeleta manufaa makubwa na kukubaliana kwamba Wataalamu wetu wa Idara ya Ardhi kushirikiana kupitia upya maeneo yetu ya Kiutawala hasa tunapoeleke kwenye Chaguzi Mbalimbali ikiwa ni pamoja na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na uchaguzi Mkuu 2025

Hata hivyo Mkurugenzi huyo amezishukuru Kamati za Ulinzi na Usalama zote mbili chini ya Wakuu wa Wilaya akiwepo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Elibariki Bajuta Mkuu wa Wilaya ya Urambo na Dkt. Rashid Chuachua Mkuu wa Wilaya ya Kaliua kwa kusimamia vyema kikao hiko huku wakiwemo Viongozi wengine mbalimbali kwa Ushirikiano mwema kuwahudumia Watanzania kwa ufanisi mkubwa.

" Binafsi nizishukuru Kamati zote mbili za Ulinzi na Usalama za Wilaya zetu chini Wakuu wa Wilaya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Elibariki Bajuta Mkuu wa Wilaya ya Urambo na Dkt. Rashid Chuachua Mkuu wa Wilaya ya Kaliua kwa kusimamia vyema kikao chetu kimeenda vizuri na Viongozi wenzangu kwa Ushirikiano mwema kuwahudumia Watanzania kikamilifu " amefafanua Quintine.

Mkurugenzi huyo pia amemshukuru Mh.Rias Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna ya kipekee ya kuendelea kuwapatia Miradi Mbalimbali ya Maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Urambo na Kaliua.

" Urambo ni kati ya Wilaya 7 zinaOunda Mkoa wa Tabora, ilianzishwa Julai 17,1975, Makao Makuu ya Wilaya hii yapo katika Mji Mdogo wa Urambo katika umbali wa km.90kutoka Tabora Mjini" amesema Grace Quintine.

Akizungumzia Uchumi wa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Quintine amesema Uchumi wao inategemea zaidi kwenye kilimo ambacho kinaajiri takribani asilimia 80 ya Wakazi wote wa Wilaya hiyo, ambapo mapato yao yanatokana na ufugaji, uvuvi, ufugaji wa nyuki, na shughuli za viwanda vidogo vidogo ambavyo ni ajira mbadala zinazochangia pato la wakazi hao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...