Na Mary Margwe

Mbunge wa Jimbo la Kiteto Mkoani Manyara Mh. Edward Lekaita, amemuomba Waziri wa Habari , Mawasiliano na Teknolojia ya habari Mh.Nape Nnauye kuhakikisha analipa deni la sh.Bil.18 zinazodaiwa na vyombo vya habari mbalimbali hapa Nchini

Hayo amezungumza Mei 16,2024 wakati akichangia kwenye Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya habari iliyowasilishwa na Waziri husika.

Mh.Lekaita amesema Wabunge wengi wamezungumziansuala la Uhuru wa vyombo vya habari na kweli Uhuru upo isipokua Kuna vyombo vya habari vinadai, hivyo Uhuru wa vyombo vya habari uhamie kwenye kulipa hayo ,adeni ya sh.bil.18.

" Nadhani ni kidogo sana, Mh.Nape wewe huwezi kushindwa kulipa sh.bil.18, mlipe ili Sasa huu Uhuru ,liowapa wakafanye kazi, bila kulipa haya madeni sasa hivi uhuru mnawapa alafu hawana pesa, hebu muwasaidie na mimi najua wewe unafanya kazi nzuri sana, na mmetuambia hapa Mh.Waziri kuwa nchi imetoka kwenye nchi zenye uhuru wa vyombo vya habari kutoka mia Moja arobaini na kitu hivi hadi kufikia 94" amesema Mh.Lekaita.

Aidha Mbunge Lekaita amesema " Kwa nchi yetu ya Tanzania yenye sifa nyingi sana bado hebu peleka tena mbele zaidi maana ni chache tunataka kwasababu kwenye ilani ya CCM nilikua nasoma hapa ukurasa wa 175 inasema habari ni moja kati ya haki msingi za binadamu, kwakua kila mwananchi anayo haki ya kutoa na kupokea habari, na kwasababu Ilani imeweka vizuri nadhani tuendelee tuwapite wengine, nchi yetu iendelee kuleta maraki huko Duniani" ameongeza Mbunge Lekaita.

Aidha pia amesema anakubaliana na Wabunge wenzake waliopita kuchangia kuwa nchi lazima ijengwe kwa kodi, ambapo amesema Ili nchi iweze kuwa na makusanyo mazuri ya Kodi lazima iondolewe mikono ya watu katika makusanyo ( Cash Money)

Aidha Lekaita amempongeza Mh.Rais Samia Suluhu Hassan kwa kusaidia Wizara hiyo, ameona pesa zimeongezeka nanubunifu pia Imeongezeka .

" Minara 758 ni mradi mzuri sana imegusa kila mahali, Manyara iko jumla ya Minara 33 kati ya hiyo 12 Iko Kiteto, na kati ya hiyo 12 Minara 6 imeshaanza kufanya kazi,

" Tunachoomba tu Mh.Waziri na nilishazungumza hapa Kiteto tulikua hatuipati Redio Tanzania ,mlakini nashukuru sana kwamba kwenye bajaeti yako kati ya Wilaya ambazo mmeweka kufikia ni Kiteto, hivyo wananchi wa Kiteto watafarijika sana kuanza kupata Redio Tanzania, waanze kufuatilia mambo ya Taifa lao Kwa ukaribu zaidi" ameongeza Mh. Edward Lekaita.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...