Na Patricia Kimelemeta


WAKAZI wa Kijiji cha Kisaki kilichopo mkoani Morogoro wamesema kwasasa wameacha ujangiri baada ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kupitia Hifadhi ya Nyerere kutoa ufadhiri wa masomo ya elimu ya juu na kati kwa vijana zaidi ya12 pamoja na ufadhiri wa fedha mbegu katikka vikundi 15 vilivyopo kwenye Kijiji hicho.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wakazi hao wamesema kuwa, TANAPA kupitia Hifadhi ya Nyerere imewainua kiuchumi wakazi wa eneo hilo  kupitia miradi ya ujirani mwema inayotekelezwa na Shirika Hilo ya regrow, vikundi vya uhifadhi vya jamii (Cocoba) na ufadhiri wa masomo wa ngazi tofauti ya elimu ya juu na kati.

" Awali kabla tanapa hawajaja, tulikua tunafanya shughuli za uwindaji kinyume na utaratibu, kwa sababu ya hali ngumu ya maisha na kwamba tulikua hatujui umuhimu wa wanyama pori...

"Lakini walipokuja TANAPA kupitia Hifadhi ya Taifa ya Nyerere wameweza kutuelimisha  na kuona umuhimu wa  wanyamapori, tumekuwa mabalozi na walinzi,"amesema Omary Khamis mkazi wa Kijiji hicho.
Ameongeza licha ya kupewa elimu hiyo, pia  wamekuwa wakishirikiana na wafanyakazi wa hifadhi hiyo katika shughuli mbalimbali za maendeleo, jambo ambalo limewasaidia kuwainua kiuchumi.

Mkazi mwingine Khalid Hamidu amesema kuwa, tangu Hifadhi ya Nyerere ilipoanzishwa,TANAPA imekua mstari wa mbele kuwaletea wananchi maendeleo kupitia kwenye miradi ya regrow,  vikundi Cocoba  na ufadhiri kwa vijana wanaomaliza elimu ya msingi na sekondari.

" Miradi yote hiyo mnaomba wenyewe kupitia maandiko yenu, kuna baadhi ya vijiji waliomba kujengewa madarasa ya shule za msingi na sekondari, nyumba za walimu, vyoo na kadhalika, kuna wengine waliomba miradi ya afya wajengewe zahanati 

"Na sisi tuliomba fedha na mbegu kwa ajili ya kuanzisha vikundi vya kuweka na kukopa kupitia Cocoba ambapo zaidi ya  Sh.milioni 150 zimetumika," amesema Hamidu na kuongeza kutokana na hali hiyo, wananchi wanaoishi pembezoni kwa hifadhi wamekuwa na maisha bora kuliko ilivyokuwa awali.

Kwa upande wake Ofisa Uhusiano wa Jamii kutoka Hifadhi ya Taifa ya Nyerere, Innocent Happymack amesema kuwa, TANAPA kupitia hifadhi hiyo imekuwa ikitekeleza miradi ya kijamii katika vijiji vinavyozunguka hifadhi 

"Wananachi wanatakiwa kuleta andiko ambalo litatokana na vikao vya vya vijiji Kwa kuangalia mambo wanayoyataka, halafu wanaleta kwetu na sisi tunawasiliaha kwenye mamlaka husika kwa ajili ya utekelezaji.
"Ndiomaana unaona kija Kijiji kina maombi tofauti, Kuna wengine waliomba wajengewe zahanati, wengine waliomba ufadhiri wa masomo na wengine waliomba kujengewa madarasa, nyumba za walimu na matundu ya vyoo," amesema Happymack.

Ameongeza kutokana na utekelezaji wa miradi hiyo Hali ya kiuchumi wa wananachi wanaozunguka Hifadhi hiyo imrbadilika tofauti na hapo awali, wengi wameondoka kwenye dimbwi la umaskini na kuanza kupata kipato Cha ziada.

Amesisitiza Hifadhi ya Nyerere itaendelea kushirikiana na wananchi hao kwa kuwapa elimu Ili waweze kutumia rasilimali walizonazo vizuri jambo ambalo litazidi kuwa ongezea kipato na kuwainua kiuchumi.







 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...