Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zitaendelea kuweka mazingira mazuri kwa kuziimarisha Taasisi za Ujenzi ili kuhakikisha wataalamu wazawa wanakuza taaluma zao na kushiriki kikamilifu katika Ujenzi wa Miradi inayojengwa na Watanzania.

Hayo yamesemwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla katika ufunguzi wa mafunzo ya kuwaendeleza wataalamu wa Usanifu, Uhandisi na Wakadiriaji Majengo Tanzania hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Viwanja vya Maonesho Nyamanzi Wilaya ya Magharibi “B” Unguja.

Amesema kuwa Serikali zote mbili zimetoa kipaombele kwa wataalamu wa Ujenzi na Makampuni ya ndani ya nchi kupitia Wizara na Taasisi ambazo zimefanya jitihada maalum za kuweka Sera, Sheria na kanuni zenye vigezo rafiki ili kurahisisha maombi ya kazi za ujenzi hapa nchini.

Mhe. Hemed amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuitumia vyema nafasi waliyoipata ili kuweza kupata uwelewa mkubwa na mbinu mbali mbali za ujenzi ikiwemo utumiaji wa njia mbadala ya vyuma hasa Zanzibar ambapo kumekuwa na uhaba mkubwa wa matumizi mali zisizorejesheka kama vile mchanga na nyenginezo.

Aidha Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema matumaini makubwa ya Serikali kuwa mafunzo hayo yatasaidia kuonesha mbinu za kuhifadhi, kuitunza na kuiendeleza miji ya urithi ambayo inachangia kuongeza pato la Taifa kupitia watalii wanaokuja nchini

Sambamba na hayo ametoa wito kwa Makampuni na wataalamu wa Ujenzi kuendelea kuwa waadilifu katika kutekeleza majukumu yao ikiwemo kuzingatia ubora unaohitajika na muda wa mradi uliopangwa ili iweze kutumika kama ilivyokusudiwa na kudumu kwa muda mrefu kwa faida ya vizazi vya sasa na baadae.

Akiwasilisha Taarifa ya Wizara ya Ujenzi, Mawasiano na Uchukuzi Katibu Mkuu Wizara hio Dkt. Mngereza Mzee Miraji amesema kufanyika kwa mafunzo haya kunatokana na mashirikiano yaliyopo kwa Pande mbili za Muungano kwa lengo la kuhakikisha tunakuwa na wataalamu wabobevu hasa katika masuala ya kutunza na kuboresha Miji ya Urithi wa dunia.

Dkt Mngereza amesema ushirikiano uliopo katika Sekta za Ujenzi kwa Tanzania Bara na Zanzibar Umesaidia kuimarika kwa Miundombinu ya Barabara na kupelekea kuongezeka kwa Kipato Kwa mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla pamoja na kuimarika kwa huduma za kijamii.

Kwa upande wao Wenyeviti wa Bodi ya Usajili wasanifu, wahandisi na wakadiriaji majengo kutoka Zanzibar na Tanzania Bara wamezishauri Serikali kutumia wataalamu wazalendo katika shuhuli za ujenzi ili majengo na Miji ya Urithi iweze kuwa bora zaidi.

Wamesema wakati umefikwa kwa Serikali kuangalia sheria na miongozo katika masuala ya ujenzi ili kupunguza changamoto ya kujengwa kwa majengo yasiokidhi viwango na ubora na kuendelea kulitia hasara Taifa siku hadi siku.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akipokea maelezo kutoka kwa Meneja wa Uhusiano wa Shirika la Bandari Zanzibar Ndugu Hassan Juma Amour alipotembelea mabanda ya Maonesho kabla ya Ufunguzi wa Mafunzo ya Kuwaendeleza wataalamu wa Usanifu, Uhandisi na Wakadiriaji Majengo Tanzania iliyofanyika katika Viwanja vya Maonesho Nyamanzi Wilaya ya Magharibi "B" Unguja.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...