Na FARIDA MANGUBE MOROGORO

Watu 11 wamefariki Dunia na wengine wawili kujeruhiwa baada hitilafu iliyotokea katika mtambo wa mvuke wa kuzalisha umeme katika kiwanda Cha kuzalisha Sukari Mtibwa Suger kilichopo Tuliani Wilayani Mvomero Mkoa wa Morogoro

Kwa mjibu wa Kamanda wa zimamoto na uokoaji Mkoa wa Morogoro, Shabani Marugojo amesema tukio hilo limetokea Saa 7:30 Usiku kuamkia leo Mei 23, 2024, huku chanzo bado hakijafahamika

"kulitokea hitilafu katika mtambo wa mvuke wa kuzalisha umeme Waliofariki ni Wataalamu wa Umeme na Mitambo ambao walikuwa kwenye chumba cha kudhibiti mitambo hiyo" amesema Kamanda huyo

Amesema kati ya waliofariki kuna Raia watatu wa kigeni kutoka Kenya, India na Brazil ambapo miili ya wote waliopoteza Maisha imehifadhiwa Hospitali ya Mtibwa Sugar huku majeruhi wawili wakiwa wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Misheni ya Bwagala.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...