Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba amekutana na kuzungumza na Waziri wa Nchi wa Japan anayeshughulikia Mambo ya Nje Mhe. Kiyoto Tsuji katika ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam.

Viongozi hao katika mazungumzo yao wamekubaliana kuendelea kushirikiana na kufanya kazi kwa karibu kwa manufaa ya nchi na wananchi wake.

Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Waziri Makamba ameishukuru Serikali ya Japan kwa kuendelea kuwa mdau mzuri wa maendeleo kwa Tanzania ambapo imekuwa ikiipatia Tanzania misaada mbalimbali ambayo imekuwa mchango chanya kwenye maisha ya Watanzania wengi na hivyo kusaidia jitihada za Serikali kufikia maendeleo makubwa ya kiuchumi na kuhakikisha maisha bora kwa wananchi wake.

Ametaja misaada ambayo Tanzania inapokea kama misaada kutoka Serikali ya Japan kuwa ni pamoja na miradi ya ujenzi wa, barabara ya mzunguko ya Dodoma, barabara ya Holili Arusha na Soko la Malindi Zanzibar kuwa ni miongoni mwa maeneo ambayo Tanzania imenufaika nayo kupitia uhusiano na ushirikiano na Japan.

“Nitumie nafasi hii kuishukuru Serikali ya Japan kwa kukubali kwake mradi wa Upanuzi wa bandari ya Kigoma ambao utaiunganisha Tanzania na Mashariki mwa nchi ya DRC pamoja na Zambia na Burundi ambazo pia ni watumiaji wa Ziwa Tanganyika,” alisema Mhe. Waziri.

Amesema Tanzania imejipanga kuhakikisha inaongeza kiwango cha biashara na uwekezaji kati yake na Japan na hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi kwa manufaa ya pande zote mbili.

Amesema Tanzania na Japan zimekuwa zinashirikiana kupitia maeneo ya elimu kwa kusiadia kujenga uwezo kwa Watanzania, afya, miundombinu, nishati jadidifu Diplomasia na ushirikiano wa kimataifa.

Naye Mhe. Tsuji ameeleza utayari wa Japan kuendelea kushirikiana na Tanzania na kuendelea kushirikiana kuimasrisha uhusiano mzuri uliopo kati yan chi hizo.

Ameipongeza Tanzania kwa kuwa mstari wa mbele katika masuala ya amani duniani kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa na nchi nyingine na hivyo kutoa mchango mkubwa kwa uwepo wa amani na usalama duniani.

Amesema Japan iko tayari kuendelea kushirikiana na Tanzania na kuongeza biashara na bara la Afrika, kushirikiana kukuza ushirikiano na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia .







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...