Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba (Mb.) amekutana na kuzungumza na Balozi wa Switzerland nchini Mhe. Didier Chassot leo tarehe 7 Mei 2024 katika Ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam.

Katika Mazungumzo yao viongozi hao wamejadili namna kukuza na kuimarisha ushirikiano katikaSekta ya ulinzi na usalama kwa maslahi ya pande zote mbili na Jumuiya ya Kimataifa.

Pia wamejadili jinsi ya kujenga uelewa wa pamoja kuhusu athari za migogoro inayojitokeza sehemu mbalimbali duniani na kutoa mapendekezo yenye tija kwa jumuiya ya kimataifa juu ya namna bora ya kutatua migogoro hiyo ili kupunguza adhari zake kwa jamii.

Aidha wamejadili programu mbalimbali zitakazochagiza kuimarika kwa ushirikiano huo ikiwemo ziara za mara kwa mara za viongozi wa sekta ya ulinzi na usalama na kuanda na kushiriki katika mikutano inayolenga kutatua migogoro.

Akizungumza katika mkutano huo Waziri Makamba ameeleza kuwa majadiliano ya utatuzi wa migogoro ni muhimu yakaangazia Bara la Afrika ambapo kwa muda mrefu Nchi nyingi kama vile DRC zimekuwa katika migogo na hazipewi kipaumbele katika mijadala ya kuleta amani inayojitokeza katika majukwaa mbalimbali ya Kimataifa.

Naye Balozi Chassot amesema Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika utatuzi wa migogoro na kuchangia jitihada za kuleta amani sehemu mbalimbali duniani na Switzerland inaitazama Tanzania kama mdau muhimu wa kushirikiana naye kati eneo hilo.

Balozi Chassot ametoa pole kwa Watanzania kwa hasara na uharibufu uliojitokeza kutokana na athari za mvua kubwa zilizosababisha mafuriko katika sehemu mbalimbali nchini na kusababisha vifo,majeruhi, uharibu wa makazi na mali za watu na miundombinu.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akimsikiliza Balozi wa Switzerland nchini Mhe. Didier Chassot kwenye mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam, Mei 7, 2024.




aziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akifafanua jambo wakati wa mazungumzo na Balozi wa Switzerland nchini Mhe. Didier Chassot yaliyofanyika katika Ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam, Mei 7, 2024.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba na Balozi wa Switzerland nchini Mhe. Didier Chassot wakibadilishana mawazo muda mfupi baada ya mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo yakiendelea

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...