Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Tanzania, Mhe. Prof. Adolf Mkenda Jumatatu ya tarehe 27.05.2024, Ametembelea Banda la Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar na kuweza kupata maelezo ya kina kuhusu Bunifu zilizofanywa pamoja na kazi zinazofanywa na Mamlaka ya Mafunzo ya Amali,, ambapo maelezo hayo yalitolewa na Mkurugenzi Vyuo na Mafunzo wa Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Mhandisi Abdllah Mohamed Hambaly, Alipofika kutembelea katika Banda la Maonesho la MMA katika Ufunguzi wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu,Ujuzi na Ubunifu, yanayofanyika katika viwanja vya shule ya Sekondari Popatlal Jijini Tanga.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Tanzania Mhe. Prof. Adolf Mkenda pamoja na Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi wakipata maelezo kutoka kwa kwa Mkurugenzi Vyuo na Mafunzo wa Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhandisi Abdalla Mohamed Hambal (wa kwanza kulia) walipotembelea banda la Mamlaka ya Mafunzo ya Amali , kwenye Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayofanyika jijini Tanga katika viwanja vya Shule ya Sekondari Popatlal. Wa kwanza kushoto ni  Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Tanzania Mhe. Prof. Adolf Mkenda akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Vyuo na Mafunzo wa Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhandisi Abdalla Mohamed Hambal (wa kwanza kulia) alipotembelea banda la Mamlaka ya Mafunzo ya Amali , kwenye Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayofanyika jijini Tanga katika viwanja vya Shule ya Sekondari Popatlal. Wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...