Na Jane Edward,Arusha

Arusha .Zaidi ya wanunuzi 600 kutoka nchi 40 wanatarajiwa kuhudhuria maonyesho ya utalii ya Karibu Kilifair yatakayofanyika juni 7 hadi 9 katika viwanja vya Magereza Mkoani Arusha .

Aidha maonyesho hayo yanatarajiwa kuwakutanisha wadau mbalimbali wa utalii kutoka ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kuhudhuria maonyesho hayo.

Mkurugenzi na Mwandaaji wa maonyesho hayo ya Dominic Shoo amesema maonyesho yatawakutanisha waonyeshaji na wadau wa utalii 468 kutoka nchi 37 huku yakilenga kuinua chachu ya utalii kutokana na Arusha kuwa lango kuu na kitovu kikubwa cha utalii.

Amesema kuwa,kutokana na ukuaji mkubwa wa sekta hiyo ,maonyesho hayo yamelenga kuinua mazao mapya na kuuleta ulimwengu kwa pamoja kibiashara kwani maisha yamebeba thamani kubwa.

Aidha ametaja baadhi ya Mataifa ambayo yatashiriki katika maonyesho hayo ambayo ni pamoja na Ujerumani,Afrika kusini,uingereza, Italia ,Asia,na mataifa mengi ambapo mgenirasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa maliasili na utalii Angelah Kairuki.

Kufanya maonyesho siyo kitu rahisi na ni kitu cha gharama kubwa,katika kuandaa maonyesho hayo ,lengo kubwa ni kuhakakikisha wanunuzi na waonyeshaji wananufaika na maonyesho hayo"amesema

Aidha amefafanua kuwa, viingilio kwa mwaka huu kwa watu wazima ni shs 10,000 huku watoto ni ikiwa ni shs 5000, huku akitoa wito kwa Watanzania kuja kuona na kutembelea maonyesho hayo kwani ni muhimu kwa ajili ya kupata elimu mbalimbali ikiwemo sekta ya utalii, Biashara,masuala ya kifedha nk.

Kwa upande wake Daniel Sambai kutoka Serena hotel amesema kuwa, kila mwaka ongezeko la wanunuzi limekuwa likiongezeka kutoka nchi 34-40 na hii ni kutokana na uongozi na usimamizi imara wa waandaji hao ambao umekuwa mkubwa .

"Naupongeza uongozi wa Karibu Kili fair kila mwaka wanunuzi wanaongezeka na cha msingi nisema tuu wakija wanunuzi Wazuri wanachangia kuleta wageni wengi Nchini na nchi zimeendelea kuongezeka."amesema .

Naye Mkuu wa kitengo cha masoko na mauzo kutoka kampuni ya Media works Noel Petro ,amesema asiilimia 70 ya wateja wao wanatokana na utalii na ndiyo maonyesho ya kipekee sana huku akiiomba serikali kujengwa kwa mabanda ya maonyesho ya kudumu ili kuwepo kwa mazingira salama nyakati zote.

"maonyesho haya ni ya kipekee kwetu sisi kwani yanaleta fursa ya utalii kwani wateja wetu wakubwa wanatokana na utalii,kila mtu atakayekuja kwenye banda lao atapata punguzo kubwa la gharama na wamekuja na fursa ya kupunguza changamoto ya taka ngumu ikiwemo chupa za maji ili kuokoa mazingira"amesema .





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...