Waziri wa Ujenzi, Innocent L. Bashungwa (Mb) akiwasili katika Viwanja vya Bunge jijini Dodoma, ambapo atawasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa Mwaka wa Fedha 2024/25, Leo tarehe 29 Mei 2024.

.............

Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa ameliambia Bunge kuwa zoezi la ukusanyaji madeni ya kodi za pango kwa wapangaji wa nyumba za TBA ni endelevu, hivyo anatoa wito kwa wapangaji wote kuhakikisha kuwa wanalipa kodi zao kwa wakati kuepusha usumbufu ambao unaweza kujitokeza.

Waziri Bashungwa amesema hayo Bungeni Mjini Dodoma wakati akiwasilisha makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya ujenzi kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Waziri Bashungwa, ameeleza kuwa kwa mwaka wa fedha 2023/2024, TBA imefanikiwa kukusanya fedha kiasi cha shilingi Bilioni 4.3 kati ya shilingi Bilioni 14.35 ya fedha inazodai kama malimbikizo ya kodi za pango kwa wapangaji katika nyumba zake.

"Mhe. Spika, ukusanyaji wa madeni hayo ni maelekezo ya Bunge lako Tukufu na CAG, hivyo tunawaomba mtuvumilie wakati wa utekelezaji wa zoezi hili kwani ni zoezi endelevu" amesisitiza Waziri Bashungwa.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu Mhe. Selemani Moshi Kakoso ameishauri Serikali kubuni mfumo mpya na rahisi utakaoiwezesha TBA kukusanya madeni na iwapo Taasisi za Serikali na wapangaji wengine watachelewa kulipa, mfumo huo uweze kutoza riba kwa ucheleweshaji.

Aidha, Mhe. Kakoso ameweka wazi kuwa Kamati inasisitiza kuwa TBA iendelee kuchukua hatua kwa kuwaondoa wapangaji ambao taasisi zao zimeshindwa kulipa madeni wanayodaiwa.

Aidha, imesisitizwa kuwa zoezi la ukusanyaji madeni ya kodi za pango la nyumba kwa wapangaji wa TBA ni muhimu, litawezesha TBA kujenga nyumba zaidi kulingana na mahitaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...